Misri imemtaka balozi wa Uturuki nchini humo kuondoka mara moja na kuvunja mahusiano ya kidplomasia na taifa hilo,Katika kile ambacho serikali ya Misri imesema kuwa Uturuki kuitaka Misri kumuachia huru rais aliyeondolewa madarakani na jeshi,Mohamed Morsi..
Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Misri imesema kuwa inavunja uhusiano wa kidiplomasia na Uturuki kutokana na hatua ya taifa hilo kuingilia maswala ya ndani ya Misri.Kumekuwa na mvutano kati ya mataifa hayo mawili huku Uturuki ikiikosoa Misri kwa hatua yake ya kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mapema mwaka huu.
Nchi hizo mbili zilivunja mahusiano ya kibalozi mara baaada ya jeshi kumuondoa madarakani rais Morsi,na balozi wa Misri nchini Uturuki alirejea Cairo,licha ya mwenzake wa Uturuki kutoondoka kurudi Ankara, hivyo serikali ya kijeshi iliyoko madarakani imesema ni lazima balozi huyo aondoke ndani ya mipaka ya taifa hilo kwa kuwa nchi yake inataka kupinga maoni na mawazo ya watu wa misri.
Chanzo bbcswahili
0 comments:
Post a Comment