Friday 15 November 2013

UYFF ASEMA KWAKE CRISTIANO RONALDO BORA KULIKO IBRAHIMOVIC!

JOHAN_CRUYFFLEO KITIMTIM SAA 4 DAK 45 USIKU: PORTUGAL v SWEDEN!
LEJENDARI wa Holland Johan Cruyff, licha ya kukiri Mastaa Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic wote ni mahiri, amesema kwake ni bora Ronaldo awepo Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia kuliko Ibrahomovic.
Leo Usiku, Portugal, inayoongozwa na Ronaldo, inapambana naCR7_v_IBRA Sweden ya Ibrahimovic katika Mechi ya kwanza ya Mchujo ya kuwania kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambapo Timu hizi zitarudiana Jumanne ijayo na Mshindi wake atatua Brazil.
Lakini Johan Cruyff, ambae aliwahi kuichezea na kuifundisha Barcelona, amesisitiza ni jambo la kuhuzunisha mmoja kati ya Cristiano Ronaldo au Zlatan Ibrahimovic kuzikosa Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni Mwakani.


WASIFU: CRISTIANO RONALDO ZLATAN IBRAHIMOVIC

MIAKA: 28 32
MECHI ZA KIMATAIFA:
107 [Ya kwanza v Kazakhstan, 2003) 94 (Ya kwanza v Faroe Islands, 2001)
MAGOLI  YA KIMATAIFA: 43 46
KOMBE LA DUNIA [Kucheza]: Mara 2 (2002, 2006) Mara 2 (2006, 2010)
EURO [Kucheza]:
Mara 3 (2004, 2008, 2012) Mara 3 (2004, 2008, 2012)

MATAJI MAKUBWA: Ligi Kuu England (3), La Liga, UEFA ChampionZ Ligi

Serie A (5), Eredivisie (2) La Liga, Ligue 1, UEFA Super Cup


Cruyff, akiongea na Jarida la Algemeen Dagblad la Uholanzi, alisema: “Ni pigo kubwa kwa Kombe la Dunia kumkosa mmoja wa Wachezaji hawa wawili. Inahuzunisha. Sina chagua kati yao lakini ikibidi nichageu basi ni heri Ronaldo afuzu. Hii ni siasa kidogo kwani naishi Spain!”

RATIBA:
TAREHE SAA MJI TIMU TIMU
Nov-15 2200 Reykjavik Iceland Croatia
Nov-15 2200 Piraeus Greece Romania
Nov-15 2245 Lisbon Portugal Sweden
Nov-15 2245 Kyiv Ukraine France

RATIBA-MECHI za MARUDIANO:
[Saa za Bongo]
TAREHE SAA MJI TIMU TIMU
Nov-19 2115 Zagreb Croatia Iceland
Nov-19 2145 Solna Sweden Portugal
Nov-19 2300 Saint-Denis France Ukraine
Nov-19 2100 Bucharest Romania Greece

0 comments: