Saturday 16 November 2013

UJUMBE WA ZITTO KABWA KUHUSU WARAKA WA KUCHAFULIWA NA KUTISHIWA MAISHA


Dr. Willbrod Slaa " hatuna tatizo hata kidogo na Zitto Kabwe. Huyu ni Naibu Katibu Mkuu wetu, kama kuna tatizo jambo ambalo ameleta tutamaliza kwa mujibu wa taratibu na tutaendelea na kazi na umoja wetu"
" waraka huo mchafu umeandikwa na viongozi wa CCM na kutoka idara nyeti ya serikali" chama kitapata taarifa zao na kuanika majina yao na nafasi zao
Edwin Mtei " haya mambo hayatubabaishi, tunajua ni uongo uliotungwa ili kutugombanisha" ..."kesho unaweza kusikia Zitto amehongwa hiki au kile. Keshokutwa ukasikia Slaa amehongwa hiki baadaye Mbowe amefanya hivi. Lengo kutuvuruga"
Mabere Marando " andishi hili ni feki. Nimeliangalia andishi lote. Nimejiridhisha kwamba limetengenezwa na watu wasiotakia mema chadema"
Maneno mazuri sana yenye ukweli mtupu. Hata hivyo hekaya hii imesambazwa na wanachama wa CHADEMA na mmoja ni kiongozi wa mkoa na akaweka kwenye blogu yake. Viongozi wengine waka 'like' kwenye jamii forums. Hawa wametumwa na usalama na CCM?
Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe". Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM. Wahusika waendelee kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani. Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa tuhuma za uongo.
Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa.

0 comments: