Serikali ya Niger imetangaza kuwa itafunga kambi zote za wakimbizi kaskazini mwa nchi.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni, serkali pia ilisema kuwa wale wote wanaoshiriki katika biashara ya kuwasafirisha wahamiaji kimagendo, kwa kupitia Niger Kaskazini hadi Algeria na Libya, watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali.
Tangazo hilo limetolewa siku chache baada ya watu 92 wanaodhaniwa walikuwa wakimbizi, kupatikana wamekufa katika jangwa la Sahara - miili yao ilikuwa imeoza.
Waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Niger, Mohamed Ba-zoum, ameiambia BBC kuwa mji wa Agadez peke yake, kaskazini mwa Niger, una wahamiaji kama 5,000 kutoka sehemu mbalimbali za Afrika kwenye makambi yasiyoruhusiwa.
Chanzo bbcswahili
0 comments:
Post a Comment