Wanasiasa na watu maarufu duniani
wamesema hawatahudhuria mashindano ya Olympic ya walemavu 'Paralympic'
ya majira ya baridi nchini Urisi yaliyopangwa kufanyika katika mji wa
Sochi kutokana na hatua ya Urusi katika eneo la Crimea.
Marekani imeuondoa ujumbe wa nchi hiyo
kwenye mashindano hayo yanayofunguliwa leo. Nchi nyingine za Ulanya
zimetangaza hatua kama hiyo.
Hata hivyo bado haijafahamika kama timu ya walemavu ya Ukraine itashiriki mashindano hayo.
Ujumbe wa timu hiyo uliinua bendera ya
nchi yao wakati wa sherehe ya ukaribisho katika mji Sochi siku ya
Alhamisi lakini uamuzi kwamba watashiriki mashindano hayo au la bado
haujajulikana.
Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema nchi ambazo zimesusia tukio hilo hawana nia njema.
Chanzo: BBC swahili
0 comments:
Post a Comment