Huyu ni Germain Katanga kwa jina la utani Simba
Mahakama ya kimataifa ya jinai ICC
imempata na hatia ya uhalifu wa kivita mbabe wa kivita kutoka Jamhuri ya
kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga.
Hata hivyo Katanga hakukutwa na hatia katika shtaka la udhalilishaji wa kijinsia.
Alituhumiwa
kuhusika na mauaji ya wanavijiji zaidi ya 200 mwaka 2003 katika jimbo
la Ituri lenye utajiri wa dhahabu, kaskazini mashariki mwa Congo.
Katanga ni mtu wa pili kupatikana na
hatia ya uhalifu wa kivita katika mahakama ya ICC tangu ianzishwe mjini
The Hague, Uholanzi mwaka 2002.
Katika shambulio hilo lililotokea
mnamo Februari 24, 2003 watu 200 waliuawa katika kijiji cha Bogoro
karibu na mpaka wa Uganda,Katanga wakati huo akiwa Kamanda wa kundi la
waasi la Patriotic Resistance Force of Ituri (FRPI) lililotekeleza
mauahi hayo.
Mwendesha mashtaka amesema nia yao kuu ilikuwa kuangamiza kijiji kizima.
Germain Katanga kwa jina la utani Simba alikanusha mashtaka hayo yote dhidi yake
0 comments:
Post a Comment