“PRESS RELEASE” TAREHE 06.03.2014.
- MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.
- MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
- JI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
- JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
MPANDA BAISKELI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI MBOZI.
GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.953 BJL AINA YA NISSAN MALI YA KAMPUNI YA
USAFIRISHAJI YA SUMMRY LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA FURAHA JONAS
(32) MKAZI WA SUMBAWANGA, LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAYE SIMON
PHILIPO @ SIAME (25) MKAZI WA KIJIJI CHA CHIMBUYA NA KUSABABISHA KIFO
CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO ILITOKEA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA
SAA 17:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMBUYA, KATA YA MPEMBA,
TARAFA YA CHIMBUYA, WILAYA YA MBOZI. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI.
DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUO CHA POLISI VWAWA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI
WENGINE WA BARABARA HASA WATEMBEA KWA MIGUU KUWA MAKINI WANAPOTUMIA
BARABARA KWA KUTEMBEA PEMBEZONI MWA BARABARA NA KUVUKA KATIKA SEHEMU
ZENYE VIVUKO [ZEBRA CROSSING] ILI KUEPUKA AJALI.
MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE
MWENDESHA
PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FURAHA KASALILE (29) MKAZI WA
KIJIJI CHA KIKITA ALIYEKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI
T.969 AQY AINA YA SLG ALIGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.165 CLK
AINA YA TOYOTA NOAH ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. AJALI HIYO
ILITOKEA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 14:00HRS MCHANA HUKO
KATIKA KIJIJI CHA KIKITA, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA
RUNGWE. CHANZO CHA AJALI NI MWENDESHA PIKIPIKI KUJARIBU KUYAPITA
MAGARI YALIYOKUWA MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI. DEREVA WA GARI
ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA/KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA BHANGI.
WATU
WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. MESHACK KILUMBILE (23) NA 2. HAMZA
ABDALAH (30) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IHANGA WANASHIKILIWA NA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI UZITO WA GRAM 500. WATUHUMIWA
HAO WALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA
YA SAA 04:05HRS ALFAJIRI HUKO KATIKA KIJIJI CHA MKANYAGENI, KATA YA
RUJEWA, TARAFA YA RUJEWA WILAYA YA MBARALI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI
KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WATANO WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
WATU
WATANO WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. RAHABU SHADRACK (31) MKAZI WA
KIJIJI CHA KALASHA 2. SIKUJUA JACKSON (40) MKAZI WA KIJIJI CHA IBILILO
3. ANYASIME WILLISON (36) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA 4. LUCAS HEZRON
(25) MKAZI WA KIJIJI CHA KIWIRA 5. SIMON HEBRON (25) MKAZI WA KIJIJI CHA
KIKOTA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA KUMI [10]. TUKIO HILO LILITOKEA
MNAMO 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 13:30HRS MCHANA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LUKWEGO, KIJIJI CHA KARASHA, KATA YA KIWIRA,
TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA
MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA BHANGI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA SALVATORY MWANKENJA (34) MKAZI WA KIJIJI CHA KIKOTA AKIWA NA BHANGI
KETE NNE [04] SAWA NA UZITO WA GRAM 20. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIENDESHWA NA JESHI LA POLISI MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA
SAA 13:00HRS MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIKOTA, KATA YA KIWIRA,
TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WAKIWA NA MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI.
JESHI
LA POLISI MKOA LINAWASHIKILI WAFANYABIASHARA WAWILI 1. PHILIPO
MWAISANILA (27) MKAZI WA MAKUNGULU NA 2. KELVIN JAPHET (28) MKAZI WA
MWANJELWA WAKIWA NA MADUMU 40 YA DAWA YA KUSAFISHIA MADINI AINA YA SOLID
YAKIWA YAMEPAKIWA KWENYE GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.948 AEL AINA YA
CANTER MALI INAYODHANIWA KUWA YA WIZI. WAFANYABIASHARA HAO WALIKAMATWA
MNAMO TAREHE 05.03.2014 MAJIRA YA SAA 21:00HRS USIKU HUKO KATIKA KIJIJI
CHA KAWETERE, KATA YA MWANSEKWA, TARAFA YA SISIMBA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA
POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJIHUSISHA NA
SHUGHULI HARAMU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WATAFUTE KAZI
HALALI ZA KUFANYA ILI WAJIPATIE KIPATO NA KUENDESHA MAISHA YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU SITA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI
KATIKA
MSAKO ULIOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA MNAMO TAREHE
05.03.2014 MAJIRA YA SAA 19:00HRS JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KATUMBA,
KATA YA IBICHI, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE, WATUHUMIWA SABA
WALIKAMATWA AMBAO NI 1. GEOFREY MWAKIPESILE (41) 2. BONIFACE MWAKAMBOJA
(29) MKAZI WA KIJIJI CHA LUSANJE 3. ATHUMANI MWANKOTWA (31) 4. MOSES
ARON (21) 5. FURAHA MWANDEBI (40) 6. MUSA GEORGE (28) 7. BONIFACE
JOSEPH (19) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA KATUMBA WAKIWA NA POMBE HARAMU
YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TANO [05]. WATUHUMIWA NI WATUMIAJI NA
WAUZAJI WA POMBE HIYO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment