Picha na Saleh Jembe.com, Misri
Na Baraka Mpenja
MABINGWA
wa ligi kuu soka Tanzania bara na wawakilishi pekee wa nchi katika
michuano ya kimataifa, Dar Young Africans tayari wamewasili jijini Cairo
kujiandaa na mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Africa
utakaopigwa jumapili machi 9 mwaka huu dhidi ya mabingwa watetezi wa
kombe hilo, klabu ya National Al Ahly.
Taarifa
kutoka Misri zinaeleza kuwa baada ya wachezaji, benchi la ufundi na
viongozi wa klabu ya Yanga SC kufika uwanja wa ndege mjini humo,
waandishi wa habari walitaka kuzungumza na wachezaji, lakini hakuna
mchezaji yeyote aliyezungumza nao kwa sababu maalumu.
Waandishi
hao baada ya kuchuniwa na wanajangwani, waliishia kuwapiga picha
wachezaji, viongozi pamoja na basi walilopanda kuelekea Katika Hotel
waliyokusudia kuweka kambi.
0 comments:
Post a Comment