Taarifa
ikufikie kwamba Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kupunguza
mshahara wake na wa Makamu wake William Ruto kwa asilimia 20 na mshahara
wa Mawaziri utapunguzwa kwa asilimia 10.
President mwenyewe amesema hii ishu nzima
iliafikiwa kwenye mkutano na baraza la Mawaziri uliofanywa kwa siri
ambapo amekaririwa akisema ‘tukizingatia hali ya kupanda kwa garama mimi
na makamu wangu tunachukua hatua ya kupunguza mshahara wetu, makatibu
wakuu wa serikali na makatibu wasaidizi nao wamekubali asilimia kumi
kukatwa kwenye mishahara yao kuanzia sasa’
‘Kingine ni kwamba tutaandaa mkataba mpya wa
kusafiri ambao utafuta safari za nje ya nchi isipokua zitabaki zile
zenye umuhimu tu, serikali yangu inampango wa kupunguza matumizi
yanayojirudia na ambayo hayaongezi umaana wowote kwenye ufanyaji kazi’
CHANZO HAUBA SWAHILI KENYA
CHANZO HAUBA SWAHILI KENYA
0 comments:
Post a Comment