>>JUMAPILI MABINGWA WIGAN WAKO ETIHAD KUIVAA CITY!
WAKICHEZA kwao Emirates, Arsenal wametinga Nusu Fainali ya FA CUP baada ya kuifunga Everton Bao 4-1.
Mesut Ozil aliipa Arsenal Bao la Kwanza
katika Dakika ya 7 baada kupokea pasi toka kwa Santi Cazorla hilo likiwa
shambulio la kwanza tu kwa Arsenal.
Everton walisawazisha Dakika ya 32 kwa
Bao la Romelu Lukaku kutokana na kazi nzuri ya Kiungo Ross Barkley amabe
alikokota Mpira toka Nusu yake wa Uwanja na pasi yake kumkuta Kevin
Mirallas aliepiga shuti fyongo na Mpira kumaliziwa na Romelu Lukaku huku
Kipa Lukasz Fabianski akiwa amegaa chini.
Arsenal walipata Bao la Pili kwa Penati
ya Mikel Arteta katika Dakika ya 67, Penati ambayo ilitolewa baada Alex
Oxlade-Chamberlain kuangushwa na Gareth Barry.
Penati hiyo ilipigwa mara mbili na
Arteta kufunga ya kwanza lakini Refa Mark Clattenburg aliamua irudiwe
kufuatia Olivier Giroud kuingia ndani ya Boksi kabla haijapigwa na
Giroud kulambwa Kadi ya Njano.
Bao nyingine mbili za Arsenal zilifungwa na Olivier Giroud katika Dakika za 83 na 85.
Arsenal atamjua Mpinzani wake wa Nusu
Fainali, zitakazochezwa Wikiendi ya Aprili 12, baada ya Droo
itakayofanyika Jumapili Machi 9.
VIKOSI:
ARSENAL: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Flamini, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Özil, Cazorla, Sanogo.
Akiba: Rosicky, Podolski, Giroud, Viviano, Jenkinson, Miyaichi, Gnabry.
EVERTON: Robles, Coleman, Stones, Distin, Baines, McCarthy, Barry, Mirallas, Barkley, Pienaar, Lukaku.
Akiba: Hibbert, McGeady, Deulofeu, Naismith, Ösman, Howard, Browning.
Refa: Mark Clattenburg
FA CUP
RATIBA
ROBO FAINALI
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 9
1500 Sheffield United v Charlton
1700 Hull City v Sunderland
1905 Manchester City v Wigan
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
0 comments:
Post a Comment