Saturday, 8 March 2014

BPL MAN UNITED WAIPIGA WEST BROM MABAO 3-0

>>NI SALAAM SPESHO KWA LIVERPOOL ZA MACHI 16 OLD TRAFFORD!


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi Machi 8
[Saa za Bongo]
West Brom 0 Man United 3
1800 Cardiff v Fulham
1800 Crystal Palace v Southampton
1800 Norwich v Stoke
2030 Chelsea v Tottenham

MABINGWA wa ENGLAND, Manchester United, wakicheza Ugenini huko The Hawthorns, wameichapa West Bromwich Albion Bao 3-0 na kupanda Nafasi moja na kukamata Nafasi ya 6.
Bao la Kwanza la Man United lilifungwa kwa Kichwa na Phil Jones katika Dakika ya 34 kufuatia Frikiki ya Robin van Persie.
Frikiki hiyo ilitolewa baada ya Chris Brunt kimkata Rafael.

DONDOO MUHIMU [Toka OPTA]:
-MSIMU HUU, MAN UNITED IMECHEZESHA KIKOSI TOFAUTI KATIKA KILA MECHI YA MECHI ZAO ZOTE 42!!

MAN_UNITED_v_WBA8MAR-2Dakika ya 41, Kipa wa WBA, Ben Forster, aliunawa Mpira nje ya Boksi na kama Refa Jonathan Moss angeashiria ni Faulo ni wazi Kipa huyo aliewahi kuidakia Man United ingebidi apewe Kadi Nyekundu.
Man United walifunga Bao la Pili kupitia Wayne Rooney kwa Kichwa katika Dakika ya 65 alipounganisha Krosi ya Rafael baada muvu aliyoanzisha mwenyewe na kumhusisha Juan Mata aliempa Rafael.
Bao la Tatu lilifungwa na Danny Welbeck baada ya gonga safi ya Pasi 7 zilizomfikia Rooney aliempenyezea Welbeck na kufunga katika Dakika ya 82.
Mechi inayofuata kwa Man United ni Jumapili Machi 16 Uwanjani Old Trafford watakapocheza na Mahasimu wao wa Jadi, Liverpool.
VIKOSI:
WEST BROM: Foster; Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell; Yacob, Mulumbu; Amalfitano, Gera, Brunt; Anichebe
Akiba: Myhill, Morrison, Thievy, Vydra, Sessegnon, Dawson, Berahino.
MAN UNITED: De Gea; Rafael, Smalling, Jones, Evra; Mata, Carrick, Fellaini, Januzaj; Rooney, van Persie
Akiba: Lindegaard, Giggs, Vidic, Young, Welbeck, Fletcher, Kagawa.
Refa: Jonathan Moss

MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Chelsea 28 30 63
2 Liverpool 28 38 59
3 Arsenal 28 24 59
4 Man City 26 42 57
5 Tottenham 28 4 53
6 Man United 28 12 48
7 Everton 27 11 48
8 Newcastle 28 -2 43
9 Southampton 29 1 39
10 West Ham 28 -4 31
11 Aston Villa 28 -7 31
12 Hull 28 -5 30
13 Stoke 28 -14 30
14 Swansea 28 -4 29
15 Norwich 28 -22 28
16 Crystal Palace 27 -18 27
17 West Brom 28 -11 25
18 Sunderland 26 -16 24
19 Cardiff 28 -30 22
20 Fulham 28 -34 21
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi Machi 15
1545 Hull v Man City
1800 Everton v Cardiff
1800 Fulham v Newcastle
1800 Southampton v Norwich
1800 Stoke v West Ham
1800 Sunderland v Crystal Palace
1800 Swansea v West Brom
2030 Aston Villa v Chelsea
Jumapili Machi 16
1630 Man United v Liverpool
1900 Tottenham v Arsenal

0 comments: