>>NIKE v ADIDAS NI PIA MESSI v RONALDO, BRAZIL v SPAIN!
NIKE itazivisha Timu nyingi Jezi kupita Adidas kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni.
Makampuni hayo makubwa ya Vifaa vya
Michezo yanazipambanisha Brazil v Spain, Cristiano Ronaldo v Lionel
Messi katika vita yao ya kuibuka nani anateka Soko la Dunia la Jezi na
Buti za Soka.
Kila mmoja anatamba yeye ni Nambari Wani
lakini Wachunguzi wanadai Nike ndio wenye kampeni kabambe ya kuliteka
Soko la Soka ambalo litawaingizia Fedha nyingi kupita Mpira wa Vikapu
ambao ndio uliwatumbukiza wakawa Magwiji kwenye Soko la Dunia.
Adidas ya Germany ndio Kampuni ya asili kwenye Soka na ndio Mdhamini rasmi wa Kombe la Dunia.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko
Brazil, Nike itazivisha Timu 10 ambazo ni Australia, Brazil, Croatia,
England, France, Greece, Netherlands, Portugal, South Korea na United
States.
Adidas watakuwa na Timu 8, toka 10 za
Mwaka 2010, ambazo ni Spain, Argentina, Colombia, Germany, Japan,
Mexico, Nigeria na Russia.
Huko Brazil, Nike watamvalisha Messi na Mchezaji mwenzake wa Barcelona, Buti zao mpya ‘Magista’.
Adidas nao watamtangaza Nahodha wa
Portugal, Cristiano Ronaldo, anaecheza Real Madrid, na Straika wa
Liverpool anaecheza Uruguay, Luis Suarez, wakiwa na Buti mpya
‘Primeknits FS’ huko Brazil
0 comments:
Post a Comment