>>JUMAPILI MABINGWA WIGAN WAKO ETIHAD KUIVAA CITY!
FA CUP
RATIBA
ROBO FAINALI
[Saa za Bongo]
Jumamosi Machi 8
1545 Arsenal v Everton
PATA TATHMINI/DONDOO:
Hali za Timu
Arsenal watacheza bila Kiungo Jack Wilshere ambae alivunjika Mguu kwenye Mechi ya England na Denmark Juzi Jumatano.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger,
amegusia kuwa Sentahafu Laurent Koscielny yuko fiti lakini Aaron Ramsey
na Kim Kallstrom bado ni Majeruhi.
Nahodha wa Everton, Phil Jagielka, ana
hatihati kubwa ya kucheza akikabiliwa na tatizo la Musuli za Pajani
[Hamstring] lakini Beki mwenzake, Antolin Alcaraz, yuko tayari kurejea
baada kuwa nje Gemu 6 akikabiliwa na tatizo la Musuli.
Tathmini
Arsenal walifungwa 1-0 na Stoke City
Wikiendi iliyopita kwenye Mechi ya Ligi Kuu England lakini Wenger
anategemea Timu yake kuibuka na ushindi ili waendelee kwenye mbio za
kutwaa Kombe lao la kwanza tangu Mwaka 2005.
Wenger amesema: “FA CUP ni moja ya vitu muhimu kwetu! Tulihuzunishwa kufungwa na Stoke na ni muhimu kushinda Mechi hii!”
Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez,
ambae Timu yake ilitoka Sare ya 1-1 na Arsenal kwenye Ligi Mwezi Desemba
Uwanjani Emirates, anaamini Timu yake ipo kwenye wakati mbaya kucheza
na Arsenal wakati huu.
Amesema: “Itakuwa Gemu ya kusisimua! Wao
kucheza Nyumbani ni kitu kikubwa na watajaribu kila kitu kushinda Mechi
hii baada ya kufungwa Mechi iliyopita! Pengine huu ni wakati mbaya
kucheza nao!”
Dondoo muhimu
-Arsenal na Everton wamekutana mara 3 tu kwenye FA CUP na mara ya mwisho ni 1981.
-Everton wameshinda mara 2, Miaka ya 1910 & 1981, na Arsenal mara 1, Mwaka 1928.
-Everton hawajashinda hata Mechi moja
Nyumbani kwa Arsenal katika Mechi 19 zilizopita na Rekodi ni Ushindi: 0,
Sare: 4 Kufungwa: 15 lakini wameambua Sare 2 katika Mechi zao 2 za
mwisho.
-Roberto Martinez alikuwa Meneja wa Wigan Athletic ilipotwaa FA CUP Msimu uliopita.
VIKOSI VINATARAJIWA
ARSENAL [Mfumo: 4-2-3-1]:
-Szczesny
-Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs
-Arteta, Oxlaide-Chamberlain
-Cazorla, Ozil, Podolski
-Giroud
EVERTON [Mfumo: 4-2-3-1]:
Howard
-Coleman, Stones, Distin, Baines
-McCarthy, Barry
-Deulofeu, Osman, Pienaar
-Naismith
Refa: Mark Clattenburg [Mechi: 29, Kadi Nyekundu: 1 Kadi za Njano: 95]
FA CUP
RATIBA
ROBO FAINALI
[Saa za Bongo]
Jumapili Machi 9
1500 Sheffield United v Charlton
1700 Hull City v Sunderland
1905 Manchester City v Wigan
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
TAREHE ZA RAUNDI:
-NUSU FAINALI: Jumamosi Aprili 12 & Jumapili Aprili 13
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
0 comments:
Post a Comment