Mshindi wa tuzo ya Oscar, Lupita Nyong’o, Jana (March 5) alihudhuria kwenye maonesho ya
mitindo
ya wiki yaliyofanyika Paris inayojulikana kama ‘Miu Miu Fashion Show’,
ambapo mastaa wengi walihudhuria ikiwa ni pamoja na Rihanna.
Rihanna alikutana na Lupita Nyong’o ambapo walikaa pamoja na kupiga picha kadhaa ambazo zilipostiwa na Lupita Nyong’o.
Kwa
mujibu wa ripoti, wawili hao ndio waling’ara zaidi kimavazi katika show
hiyo, huku Lupita akionekana kuwa mchangamfu na kuzitumia dakika 40 za
mwanzo zilizoongezwa kwa ajili ya kumsubiri Rihanna kujitambulisha
vizuri kwa wageni wengine waliokuwa wamekaa nae kwenye viti vya mbele.
Baada
ya picha hiyo, wengi walianza kutoa maoni yao kwenye mitandao wakidai
wanatamani kumuona Lupita Nyong’o kwenye video moja ya wimbo wa Rihanna!!!!
0 comments:
Post a Comment