Misao
Okawa, ambaye aliwekwa kwenye kitabu cha rekodi kubwa za dunia
‘Guinness’ mwaka jana kama mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi
duniani, jana (March 5) amefanya sherehe ya siku ya kuzaliwa baada ya kufikisha umri wa mika 116.
Misao
ambaye anaishi chini ya uangalizi na matunzo huko Osaka, Japan
alitangazwa rasmi kuwa mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani baada
ya aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kufariki.
Ingawa umri wake ni mkubwa sana, anaonekana bado ana afya nzuri na aliweza kuipuliza mishumaa yake kama mtu mwingine.
0 comments:
Post a Comment