Bunge la Urusi limeidhinisha ombi la Rais Putin kuwa wanajeshi wa Urusi watumike Ukraine.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya
Urusi imesema hiyo haimaanishi kuwa wataanza kutumika moja kwa moja,
ingawa wakuu wa Ukraine wanasema Urusi imeshatuma wanajeshi 6,000 zaidi
huko Crimea.
Kikosi cha wanamaji wa Urusi katika
Black Seakimesema kuwa wanajeshi wake wanapiga doria pamoja na wenyeji
wa Crimea wanaounga mkono Urusi, ili kulinda vituo vyake.
Mwandishi wa BBC alioko Sevastopol anasema wanajeshi wanaonekana zaidi.
Meli za Ukraine za kulinda pwani
zimeondoka kuepuka kuchukuliwa na Urusi na mwandishi wa BBC anasema kuna
hisia kuwa ras wa Crimea inazidi kuwaponyoka wakuu mjini Kiev.
Chanzo, bbcswahili.com
0 comments:
Post a Comment