Wednesday, 5 March 2014

HIKI NDICHO ALICHOSEMA RAISI WA BARCELONA KUHUSU MKATABA MPYA WA LIONEL MESSI

374721_heroa 
Miezi kadhaa baada ya Cristiano Ronaldo kupewa mkataba mnono zaidi kuliko mpinzani wake Lionel Messi, raisi wa klabu ya Barcelona  Josep Maria Bartomeu amesema kwamba Lionel Messi atasaini mkataba mpya mnono na Barca mwishoni mwa msimu utakaomfanya awe mwanasoka anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani.
Boss huyo wa Barca amesema nia ya klabu  ni kuendelea kuwa na Messi kwa muda mrefu na ndio maana lengo kwa sasa ni kumshawishi Messi, mwenye miaka 26 kuendelea kubaki Camp Nou.
“Tunataka kumfanya mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani na mpaka kufikia mwishoni mwa msimu kila kitu kitakuwa sawa,” Bartomeu alikaririwa na  AS.
“Hatutomuuza. Yupo nasi na matumaini ni kwamba atastaafu soka akiwa hapa.”

Related Posts:

0 comments: