RPC Iringa
Mwandishi Diana Bisangao wa Iringa
Watu
watatu wafariki dunia mkoani Iringa na mwingine kujeruhiwa katika
matukio manne tofauti likiwemo la Alestina Mwayiga (35) mkazi wa Mapanda
wilayani Mufindi kufariki baada ya kupigwa ngumi na mateke sehemu mbali
mbali za mwili wake.
Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake leo Kamanda wa polisi mkoani Iringa Ramadhani Mungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda
Mungi alimtaja mtuhumiwa huyo jina Tedy Kileo umri bado haujafahamika
ambaye ni mume wa marehemu ndiye aliyefanya mauaji hayo ya kusikitisha
na kukimbia.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijafahamika na mtuhumiwa wa jambo hilo anatafutwa na JESHI la polisi.Katika
tukio lingine Madaraka Teleka (18) mfugaji wa Igunga anatafutwa na
polisi kwa kosa la kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili na
kumsababishia kifo mkulima wa Igunga aitwaye Mashaka Mhembe (38).
Mungi alisema chanzo cha tukio hilo ni baada ya mfugaji huyo kuingiza ng’ombe wake ndani ya shamba la marehemu.
Tukio lingine mtu mmoja amefariki dunia
na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wamepanda aina ya
Noah lenye namba za usajili T.876 BZN mali ya Ally Makula mkazi wa Mbeya
lililokuwa likiendeshwa na Emmanuel Benjamini (37) kuacha njia na
kupinduka maeneo ya Kijiji cha Mkunguru barabara kuu ya Iringa- Dodoma.
Mungi alisema tukio hilo lilitokea mnamo
tarehe 09 februari majira ya saa 10 kamili na kulitaja jina la marehemu
ni Upendo Filango (30) mkazi wa Migori, ambapo majeruhi watatu wamelazwa
katika Hospitali ya mkoa Iringa na dereva amekamatwa.
Mbali
na matukio hayo ya vifo Kamanda Mungi alisema jeshi la polisi mkoani
Iringa linamshikilia mwanamke mmoja jina Joyce Mkumbwike umri
haujafahamika kwa kosa la kumjeruhi Amoni Kyando (82) mkulima wa Kilolo
kwa kumkata na panga sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo kichwani, usoni
na mkono wa kushoto pamoja na sehemu za siri na kumsababishia maumivu
makali.
Kamanda
Mungi alithibitisha kutokea tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 06
februari majira ya saa 2 kamili usiku na kusema majeruhi huyo amelazwa
katika Hospitali ya Mafinga huku chanzo cha tukio hilo ni wivu wa
mapenzi.
0 comments:
Post a Comment