>>IVAN GAZIDIS ADAI WACHEZAJI WANALIWA FEDHA ZAO!!
Akiongea na Wanahabari baada ya Mkutano
wa ECA, European Club Association, Chama cha Klabu za Ulaya, Gazidis
alitamka: “Klabu nyingi hulipa Fedha za juu kabisa wakinunua Mchezaji na
popote Fedha hizi zinapokwenda Klabu zitalipa Fedha nyingi mno. Lakini,
Wachezaji wanapaswa kupata Fedha zaidi hasa hizi wanazolipwa Mawakala. ”
Hata hivyo, licha ya kukiri umuhimu wa Mawakala, Gazidis ametaka ziwepo Sheria mpya kudhibiti Mgao wa Fedha kwa Mawakala.
Kwa mujibu wa Utafiti wa ECA kwa Kipindi
cha Miaka miwili kuanzia 2011 hadi 2013, Mawakala walivuna Kamisheni za
Jumla ya Dola Milioni 254 ikiwa ni Asilimia 14.6 ya thamani ya Uhamisho
wa Wachezaji 865 miongoni mwa Klabu za Ulaya.
Akizungumzia ishu hii, Umberto Gandini,
ambae ni Mkurugenzi wa AC Milan na pia Makamu Mwenyekiti wa ECA,
amesema: “Tunajua lipo tatizo na upo umuhimu wa kuweka Sheria mpya
kuzuia Watu wa kati.”
Licha ya kulaumu Mgao wa Mawakala, wengi
ndani ya ECA wamekiri kuwa Taratibu za Uhamisho wa Wachezaji zilizopo
sasa zinafanya kazi barabara kama ilivyokusudiwa ambapo maslahi ya
Wachezaji na Vilabu huzingatiwa ikiwemo kuzingatiwa kwa matakwa ya
‘Hukumu ya Bosman’ ambayo humpa Haki Mchezaji Huru kwenda anapotaka bila
Klabu yake kumbana au kupata Mgao.
0 comments:
Post a Comment