Klabu hiyo Kigogo ya Italy imethibitisha
kuwa Mchezaji huyo kutoka Serbia mwenye Miaka 32 amesaini nao Mkataba
lakini hawakutoboa ni wa muda gani.
Mwezi uliopita Vidic alitangaza kuondoka
Man United baada kukaa Kipindi cha Miaka 8 na Nusu huku Meneja wa Man
United, David Moyes, akisema uamuzi huo ulikuwa wa pande zote mbili.
Ingawa inasadikiwa mwenyewe Vidic
alipendelea kubakia Man United Mkataba wake wa sasa unapokwisha mwishoni
mwa Msimu huu, lakini kwa vile hakupewa Mkataba mpya aliamua kusaka
Klabu nyingine.
VIDIC AKIWA MAN UNITED:
-25 Desemba 2005: Akubali kujiunga Man United kutoka Spartak Moscow
-25 Januari 2006: Aichezea Man United Mechi ya Kwanza v Blackburn Rovers
-Ubingwa Ligi Kuu England: 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
-UEFA CHAMPIONZ LIGI: 2008
-KOMBE LA LIGI: 2006, 2009, 2010
+++++++++++++++++++++++++++++++
Licha ya Vidic kutangaza kuondoka,
Mchezaji huyo amebaki kuwa Nahodha wadhifa ambao amekuwa nao tangu
mwanzoni mwa Msimu wa 2010/11.
Vidic alisainiwa kwa Dau la Pauni
Milioni 7 kutoka Spartak Moscow na kujenga uhusiano mzuri na Rio
Ferdinand kama Masentahafu bora kwenye Ligi Kuu England na wao ndio
waliokuwa nguzo imara ya Man United iliyotwaa Ubingwa wa England mara 3
mfululizo kuanzia 2007 hadi 2009, kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI Mwaka 2008
na kufika Fainali nyingine ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Miezi 12 baadae.
Katika Msimu wa 2008/09, Vidic alikuwepo Man United walipoweka Rekodi ya Mechi 14 mfululizo bila kufungwa hata Bao moja.
Hata hivyo, baadae akiwa Man United,
alikumbwa na majeruhi ya mara kwa mara na Desemba 2011 aliumia vibaya
Goti walipocheza huko Uswisi na FC Basel.
Hata hivyo, Vidic alifanikiwa tena
kurudi Uwanjani akiwa na Man United na kutwaa Ubingwa wa England mara
mbili zaidi na mara ya mwisho ikiwa Mei Mwaka Jana wakati Meneja wa Timu
hiyo, Sir Alex Ferguson, alipostaafu baada ya Miaka 26.
0 comments:
Post a Comment