Jaji Othman Chande
Na Nathaniel Limu, Singida
VIKAO vya mahakama kuu kanda ya kati vinatarajiwa kuanza leo februari 10 hadi machi 11 mwaka huu mjini hapa.
Akizungumza
na MOblog hivi karibuni, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi,Joyce Minde
amesema vikao hivyo vitakavyofanyika kwenye mahakama ya wazi ya hakimu
mkazi mjini Singida.
Minde amesema vikao hivyo vitakuwa chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya kati,Cresentia Makuru.
Amesema jumla ya kesi 18 za mauaji zitasikilizwa,wakati kesi zingine 19,zitasomwa katika hatua ya awali.
Minde
amesema kuwa kabla ya kuanza kwa vikao hivyo,jaji Makuru atakagua
gwaride rasmi la kuashiria kuanza kwa vikao vya mahakama kuu kanda ya
kati mkoani Singida,kwa kipindi cha mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment