Marefa France v Germany, Brazil v Colombia
FIFA imetangaza Marefa wa Mechi mbili za
Robo Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil zitalazochezwa Ijumaa
kati ya France v Germany na Brazil v Colombia.
Nestor Pitana atasimamia Mechi ya kwanza
ya Ijumaa kati ya France v Germany na hii itakuwa ni Mechi ya 4 kwa
Refa huyo kutoka Argentina kuchezesha huko Brazil.
Pitana, mwenye Miaka 39, alichezesha
Mechi za Makundi huko Brazil kati ya Russia na Korea Republic, USA na
Portugal na Honduras dhidi ya Switzerland.
Mechi ya Wenyeji Brazil na Colombia itachezeshwa na Refa wa Spain Carlos Velasco.
Velasco, mwenye Miaka 43, ameshasimamia
Mechi 2 huko Brazil ambazo ni zile za Makundi kati ya Uruguay na England
na ile ya Bosnia and Herzegovina dhidi ya Iran.
FIFA yatafakari Mchezaji Mmoja wa Akiba wa ziada kuingizwa Dakika za Nyongeza 30
Jopo la Washauri wa Masuala ya Makocha
la FIFA linatafakari kutoa mapendekezo kwa FIFA kuruhusu idadi ya
Wachezaji wa Akiba wanaotoka Benchi na kuruhusiwa kucheza iwe Wanne
badala ya Watatu wa sasa.
Lakini Jopo hilo linataka Mchezaji huyo
wa Nne atakaeruhusiwa awe anaingizwa wakati wa Nyongeza za Dakika 30
baada ya Timu kwenda Sare katika Dakika 90.
Kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard
Houllier, ambae ni mmoja wa Wajumbe wa Jopo hilo amesema: “Ni wazo zuri
ambalo tutalipeleka kwenye Vikao vya Kutunga Sheria FIFA!”
Houllier, ambae pia aliwahi kuwa Kocha
wa France, amefafanua kuwa kuruhusu Mchezaji wa 4 kuingia kwenye Dakika
za Nyongeza 30 itasaidia kupunguza athari za Wachezaji kubanwa na Musuli
wakati huo na kuzipa nafuu Timu.
Pia, Houllier amesisitiza Wachezaji
wanaotoka Benchi wana mchango mkubwa wa kubadilisha matokeo ya Mechi
kwani huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Wachezaji waliotoka
Benchi na kuingizwa wamefunga Bao 29 na kuvunja Rekodi ya Fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2006 huko Germany walipofunga Bao 23 na bado
Fainali hizi ina Mechi 8 hazichezwa.
Houllier amesema: “Wachezaji wa Akiba
wana umuhimu mkubwa kwa sababu wanaingia freshi na akili mpya. Karibu
robo ya Magoli yamefungwa kwenye Robo Saa ya mwisho huko Brazil. ”
Baadhi ya Magoli hayo ni mchango wa
Klaas-Jan Huntelaar alipoingizwa Dakika ya 76 kutoka Benchi na kuisaidia
Netherlands kwa kumpasia Wesley Sneijder Dakika ya 88 na kusawazisha na
kisha yeye mwenyewe kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa Penati ya
Dakika ya 94 walipoibwaga Mexico 2-1.
Majuzi Jumatatu, baada ya Kipa wa USA
Tim Howard kuizuia Belgium na kutoka Sare nao 0-0 katika Dakika 90,
akaingizwa Romelu Lukaku ambae, katika Dakika za Nyongeza 30, alimpasia
Kevin De Bruyne aliefunga Bao la kwanza na yeye mwenyewe kupiga Bao la
pili na Belgium kuibwaga USA 2-1.
Mwaka 2012, FIFA iliwahi kuyakataa
mapendekezo ya aina hii hii ya kuongeza Wachezaji wa Akiba kuruhusiwa
kucheza kuwa Wanne lakini safari hii Houllier anaamini yatapitishwa.
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
**Saa za Bongo
ROBO FAINALI IJUMAA, JULAI 4, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
France v Germany [57] |
ROBO FAINALI |
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro |
2300 |
Brazil v Colombia [58] |
ROBO FAINALI |
Estadio Castelão, Fortaleza |
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
1900 |
Argentina v Belgium [59] |
ROBO FAINALI |
Nacional, Brasilia |
2300 |
Netherlands v Costa Rica [60] |
ROBO FAINALI |
Arena Fonte Nova, Savador |
NUSU FAINALI JUMANNE, JULAI 8, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61] |
NUSU FAINALI |
Estadio Mineirão, Belo Horizonte |
JUMATANO, JULAI 9, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Mshindi 59 Mshindi 60 [62] |
NUSU FAINALI |
Arena Corinthians, Sao Paulo |
MSHINDI WA TATU JUMAMOSI, JULAI 12, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2300 |
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62 |
MSHINDI WA 3 |
Nacional, Brasilia |
FAINALI JUMAPILI, JULAI 13, 2014 |
|||
SAA |
MECHI |
KUNDI |
UWANJA |
2200 |
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62 |
FAINALI |
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro |
0 comments:
Post a Comment