Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia
Nkhoma Ledama, akitoa mafunzo ya maadili na jinsia kwa waandishi wa
habari na watangazaji wa Redio za Jamii nchini yanayolenga kuwajengea uwezo katika utendaji wa kazi zao kwenye vituo vyao.
Mafunzo hayo ya siku tano yamefadhiliwa na Shirika la UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na Amani kuelekea uchaguzi 2015.
Mkufunzi wa Redio za Jamii kutoka Unesco Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa
somo kwa washiriki wa Semina ya siku tano ya Maadili na Jinsia
inayolenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari na watangazaji wa Redio
za Jamii nchini iliyofadhiliwa na UNESCO kupitia mradi wa Demokrasia na
Amani kuelekea uchaguzi 2015 inayoendelea mjini Dodoma.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya watangazaji na waandishi wa habari
kutoka Redio mbalimbali za Jamii wakifuatilia mafunzo hayo yanayoendelea
mjini Dodoma.
Pichani juu na chini ni baadhi ya waandishi wa habari na watangazaji wa
redio za jamii wakichangia maoni kwenye mafunzo ya siku tano
yanayoendelea mjini Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo kutoka redio Triple A FM ya jijini
Arusha Grace Damian akizungumzia changamoto mbalimbali zinazozikabili
Redio za Jamii nchini.
0 comments:
Post a Comment