Wanakikundi
cha fataki wakitoa Igizo kwa Njia ya ushairi lililosisitiza matumizi
bora ya lugha ya Kiswahili kwa maendeleo ya lugha hiyo afrika na duniani
kwa ujumla,wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili
iliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa taifa Leo Jijini Dar es Salaam.
Wanakikundi
cha fataki wakimsalimia Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
Dkt.Fenella Mukangara(aliyesuka) wakati wa hafla ya uzinduzi Baraza
jipya la Kiswahili Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas
Mwansoko,Kushoto kwake ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza hilo Bi.Martha Qorro
na wa Mwisho ni Makamu Mwenyeki Bw. Omar Kiputiputi 
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara(kulia)akiteta jambo na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko,wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza Jipya la Kiswahili Leo Jijini Dar es Salaam. 
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akimpa
zawadi mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kutumikia Baraza la Kiswahili
Bw.Suleiman Hegga wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza jipya la
Kiswahili Leo Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
aliyemaliza muda wake wa kulitumikia Baraza la Kiswahili Bw.Suleiman
Hegga akitoa hotuba na kuwataka wajumbe wa Baraza la Kiswahili
kushikamana na kuendeleza yale waliyoanza ili kukiletea kiswahili
maendeleo Afrika na duniani kwa ujumla.katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko na Kulia ni Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara.
Wajumbe
wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) wakimsikiliza Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara wakati wa hafla
ya uzinduzi wa Baraza jipya la Kiswahili iliyofanyika katika ukumbi wa
uwanja wa taifa Leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akitoa
hotuba kwa wajumbe wa Baraza jipya la Kiswahili na kulitaka Baraza hilo
kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari katika kutoa elimu ya
matumizi fasaha ya Kiswahili sanifu ili kupunguza upotoshwaji wa
matumizi ya lugha ya Kiswahili.Kulia ni Mwenyekiti Mpya wa Baraza la kiswahili Bi.Martha Qorro
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.Fenella Mukangara akiwa
katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza Jipya la Kiswahili.
0 comments:
Post a Comment