mbunge msigwa akizungumza na wanahabari leo
mwandishi Kenneth John wa Dar
.........................................
Kutokana
na hivi karibuni
gazeti la Daily
Mail linalochapishwa nchini
Uingereza kuripoti kuhusu
biashara haramu ya
pembe za ndovu,inayokadiliwa kuwa
soko la shilingi
trilioni 19 za Kitanzania,Waziri wa
maliasili na utalii
mhe Lazaro Nyalandu
alinukuliwa na vyombo
mbalimbali vya habari
akikanusha taarifa za
chapisho hilo na
huku akisema kuwa
zilikuwa na mlengo
wa kuichafua Tanzania.
Hivyo
kutokana nakukanusha kwa
waziri Nyalandu juu ya taarifa
hizo imepelekea waziri
kivuli wa wizara
hiyo ambaye pia
ni msemaji mkuu
wa kambi ya
upinzani Mhe,Mch Peter
Msigwa kuibuka na
kusema kuwa waziri
Nyalandu amesahau kuwa
Tanzania imejichafua yenyewe
kwenye taswira ya
kimataifa kutokana na
biashara hiyo haramu
ya pembe za
ndovu.Na kuongeza Nyalandu
anasahau ulimwengu wa
sasa ni wakiteknolojia ambao
taarifa mbalimbali juu
ya biashara hiyo
haramu pamoja na
mauaji ya tembo
zimesambaa kila mahali
hasa katika vyombo
vya habari vya
ndani na nje
ya nchi .
Kutokana
na hali hiyo
Mch Msigwa amesema
kuwa anashangazwa na
waziri kutumia nguvu
nyingi katika kupangua
tuhuma dhidi ya serikali
hasa katika kushindwa
kwake katika kuangamiza
biashara hiyo haramu,Huku
akisitiza takwimu za
serikali zinaonyesha mwaka
2010 tembo elfu
kumi waliuwawa Tanzania
pekee ambapo ni
sawa na wastani
wa Tembo thelathini
na saba kwa
siku.Aidha Msigwa ameendelea
kubainisha hivi sasa
Tanzania ina Tembo
laki moja na
hamsini hadi laki
moja na sabini
na kwamujibu wa
takwimu hizo Msigwa
amesema kunauwezekano mkubwa
endapo ifikapo mwaka
2017 hadi 2018
nchi inaweza kuwa
haina tembo hata
mmoja,Hivyo Msigwa akasema
kutokana na takwimu
hizo anashaangaa kusikia waziri
akidai kuwa serikali
inachafuliwa wakati takwimu
zinaonyesha hali halisi
ya kuendelea kwa
biashara hiyo.
Aidha Mch,
Msigwa ameongeza kuwa
mara nyingi waziri
amekuwa akinukuliwa na
vyombo vya habari
akisema mtandao wa
ujangili unafahamika na
ni mpana na
unauhusisha watu wenye
nguvu za pesa
na huku akiwaomba
wanaojihusisha kuachana na
biashara hiyo mara
moja. Hivyo Msigwa akasema anachoona
hapo kwa waziri
Nyalando ni kama
anawabembeleza watuhumiwa huku
akijua fika wanavunja sheria.
Pamoja
na hayo ameendelea
kusema kauli hizo
za waziri Nyalandu
zinaonyesha dhahiri kuwa
kuna watu ambao
hawaguswi na sheria
na wapo juu
ya sheria.
Hata
hivyo Mch Misigwa
amesema kuwa kauli
hizo zinaendelea kuonyesha
kuwa mtandao huo
umekuwa ukiogopwa.
“Majibu haya
waziri yanadhihirisha kuwa
mtandao huu unaolalamikiwa na
kuogopwa ndio unaohusisha
Ikulu,wanasiasa, watumishi
wa serikali,maafisa wanyamapori,maafisa usalama,Polisi, wanajeshi
pamoja na wanyabiashara
wakubwa ambao wamekuwa
wakijihusisha na serikali
ya CCM”Alisema Mch,
Msigwa.
Akiendeendelea
kufafanua Mch Msigwa
amesema kitendo cha
kukamata kwa shehena
za meno na
pembe za ndovu
hakumaanishi kuwa waziri
anafanya kazi kwani
tembo wanakuwa tayari
wamekwisha uwawa .
Halikadharika Mch,
Msigwa amesema kuwa
serikali makini haiwezi
kumbembeleza jangili na
hali hiyo inaonyesha
serikali bado haipo makini
juu ya suala
hilo.
Sambamba
na hayo pia
amebainisha baadhi ya
tuhuma ambazo serikali
ya Tanzania ilituhumiwa
na Gazeti la
Daily Mail lakini
hazikutolewa ufafanuzi na
Waziri Nyalandu.
Tuhuma
hizo amesema ni
pamoja na watu
waliokaribu na mhe
Rais Kikwete wanahusika
katika biashara ya
meno ya tembo
ndio maana serikali
yake imekuwa haichukui
hatua stahiki katika
kukabiliana na jambo
hilo,na tuhumu nyingine
ni ile ya
ndege iliyomleta Rais
wa China kuondoka
na shehena ya
meno ya tembo
ambayo ilipakiwa na
maafisa waliokuwamo kwenye
ndege hiyo, halikadharika na
tuhuma ya kuwa
CCM serikali yake
ni wanufaikaji wakubwa
wa mradi huu
kutokana wanatafuta fedha
kwaajili ya uchaguzi
mkuu ujao na
ndio maana hawachukui
hatua kwa wahusika
ambao wanajulikana kwa
majina na wapo
mitaani wakiendelea na
biashara hiyo haramu.
Na
kutokana na tuhuma
hizo Msigwa amemtaka
Nyalandu kuondoa ukimya
na kujibu tuhuma
hizo kwa vielelezo
na si kwakuhisia
na kusema hizi
ni taarifa za
uongo pasipo kuonyesha
taarifa za ukweli.
Pamoja
na yote Mch,
Msigwa ameendelea kusema
kuwa serikali bado
haijachukua hatua za
kuridhisha katika ujangili,na
kuongeza kuwa bado
kunahali ya kulindana
na bado hatua
za makusudi hazijachukuliwa kwaajili
ya utatuzi wa
tatizo hili.
0 comments:
Post a Comment