BARCA, baada kufungwa Juzi kwenye La Liga, wamepata faraja kwa Staa wao Neymar kurejea tena Mazoezini lakini PSG wamepata pigo kufuatia kuumia kwa Fowadi wao Edinson Cavani na Anderson, alieihama Man United kwa Mkopo kwenda Fiorentina, amedai United itahamwa na Mastaa kibao.
SOMA ZAIDI:
BLANC ATHIBITISHA CAVANI NJE WIKI KADHAA!
Straika wa Paris St Germain Edinson
Cavani atakuwa nje kwa Wiki kadhaa baada kuumia Paja walipocheza na
kuifunga Bordeaux 2-0 hapo Ijumaa kwenye Mechi ya Ligue 1.
Akithibitisha habari hizo, Meneja wa PSG, Laurent Blanc, alisema Staa huyo kutoka Uruguay atakuwa nje kwa Wiki kadhaa.
NEYMAR ARUDI MAZOEZINI!!
Habari hizi zimethibitishwa na Klabu yake Barcelona ambayo imetoa taarifa kuwa Staa huyo ameanza Mazoezi ya peke yake hii Leo.
Neymar, mwenye Miaka 21, aliumia enka
yake hapo Januari 16 Barca walipocheza na kuifunga Getafe Bao 2-0 kwenye
Mechi ya Copa del Rey.
Juzi Jumamosi, Barca walifungwa Uwanjani
kwao Nou Camp Bao 3-2 na Valencia kwenye Mechi ya La Liga na kupoteza
uongozi wa Ligi ambao sasa umekamatwa na Atletico Madrid ambao wako
Pointi 3 mbele.
Jumatano Barca watakuwa tena kwao Nou Camp kucheza Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Copa del Rey dhidi ya Real Sociedad.
ANDERSON ADAI MASTAA WENGI KUIHAMA UNITED!
Anderson, ambae Wiki iliyopita alijiunga
na Fiorentina ya Italy kwa Mkopo hadi mwishoni mwa Msimu kutoka
Manchester United, amesema hana nia ya kurudi Old Trafford na pia kudai
Mastaa wengi wataihama Man United.
Kwa mujibu wa Anderson, Mastaa ambao
wataondoka Man United ni pamoja na Winga wa Ureno, Nani, ambae mwanzoni
mwa Msimu huu alisaini Mkataba mpya wa Miaka mitano na Man United.
Anderson amesema: “Nina hakika Wachezaji
wengi wanataka kuondoka, hasa mie na Nani ambao tulikuwa huko Miaka 7
au 8. Manchester United ni Klabu kubwa, Klabu inayotimiza kila kitu kwa
Wachezaji wake, lakini mara nyingine Mchezaji anataka kuhama ili kupata
uzoefu mwingine na kujifunza mengine.”
Hata hivyo, ndani ya Man United,
inajulikana kuwa Rio Ferdinand, Patrice Evra na Nemanja Vidic wanamaliza
Mikataba yao mwishoni mwa Msimu huu huku kukiwa na wasiwasi kuhusu
hatima ya Nani na Javier Hernandez ‘Chicharito.’
0 comments:
Post a Comment