Monday, 3 February 2014

ANGALIA CHELSEA ALIVYO ICHAPA MAN CITY, ARSENAL YABAKI JUU!!!


>>MAN CITY 0 CHELSEA 1!!
LIGI KUU ENGLAND
MATOKEO:
Jumatatu Februari 3
Man City 0 Chelsea 1

CITY_v_CHELSEA-FEB3BAO la shuti kali la Branislav Ivanovic katika Dakika ya 32 Jana Usiku liliipa Chelsea ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Manchester City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Man City Nyumbani kwao Etihad ambako wameshinda Mechi 11 kati ya 11 za Ligi Msimu huu.
Matokeo haya yameibakisha Arsenal kileleni mwa Ligi ikiwa Pointi 2 mbele na kuziacha City ziko Nafasi ya 2 na Chelsea Nafasi ya 3, zote zikiwa na Pointi 53 kila mmoja.
City, wakicheza bila Fernandinho na Sergio Aguero, walimalizwa na mbinu safi za Chelsea za kushambulia kwa kustukiza na wangeweza kufunga Bao nyingi zaidi kwani walipiga Posti mara 3 kupitia Samuel Eto'o, Nemanja Matic na Gary Cahill.
Man City watapata nafasi ya kulipiza kisasi kwani watakutana na Chelsea tena hapo Februari 15 Uwanjani Etihad kwenye Mechi ya Raundi ya Tano ya FA CUP. 
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Navas, Demichelis, Toure, Silva, Dzeko, Negredo
Akiba: Milner, Rodwell, Clichy, Pantilimon, Jovetic, Boyata, Lopes.
Chelsea: Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta; David Luiz, Matic; Ramires, Willian, Hazard; Eto'o.
Akiba: Cole, Lampard, Oscar, Mikel, Salah, Ba, Schwarzer.
REFA: Mike Dean
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
24
26
55
2
Man City
24
41
53
3
Chelsea
24
24
53
4
Liverpool
24
29
47
5
Everton
24
12
45
6
Tottenham
24
-1
44
7
Man Utd
24
10
40
8
Newcastle
24
1
37
9
Southampton
24
7
35
10
Aston Villa
24
-7
27
11
Stoke
24
-14
25
12
Swansea
24
-6
24
13
Hull
24
-7
24
14
Sunderland
24
-11
24
15
Norwich
24
-18
24
16
Crystal Palace
24
-18
23
17
West Brom
24
-6
23
18
West Ham
24
-9
22
19
Cardiff
24
-22
21
20
Fulham
24
-31
19
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 8
1545 Liverpool v Arsenal
1800 Aston Villa v West Ham
1800 Chelsea v Newcastle
1800C rystal Palace v West Brom
1800 Norwich v Man City
1800 Southampton v Stoke
1800 Sunderland v Hull
2030 Swansea v Cardiff
Jumapili Februari 9
1630 Tottenham v Everton
1900 Man United v Fulham
Jumanne Februari 11
2245 Cardiff v Aston Villa
2245 Hull v Southampton
2245 West Ham v Norwich
2300 West Brom v Chelsea
Jumatano Februari 12
2245 Arsenal v Man Unitwd
2245 Everton v Crystal Palace
2245 Man City v Sunderland
2245 Newcastle v Tottenham
2245 Stoke v Swansea
2300 Fulham v Liverpool

Related Posts:

0 comments: