- D
BAADA ya vipigo mfululizo kwa Wiki mbili sasa, AS Roma Jumapili wanataka kurudisha mbio zao za kuwafukuza Mabingwa na Vinara Juventus kwenye reli watakapocheza Mechi ya nyumbani na Torino.
Mapema hiyo Jumapili, Juve, ambao wako kileleni wakiwa Pointi 3 mbele ya AS Roma, watakuwa nyumbani kucheza na Parma ambao wako nafasi moja toka mkiani.
Mwendo mbovu wa AS Roma ulianzia pae walipobondwa 7-1 Uwanjani kwao Stadio Olimpico hapo Oktoba 21 na Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, na kufuatia vipigo toka kwa Napoli, bao 2-0 kwenye Serie A, na Juzi 2-0 na Bayern Munich kwenye UCL huko Munich.
Mechi za Serie A Wikiendi hii zitaanza Jumamosi kwa Mechi mbili na zilizosalia zote kuchezwa Jumapili.
SERIE A
RATIBA
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 8
2000 Sassuolo v Atalanta
2245 Sampdoria v AC Milan
Jumapili Novemba 9
1430 Cagliari v Genoa
1700 Chievo v Cesena
1700 Empoli v Lazio
1700 Juventus v Parma
1700 Palermo v Udinese
2000 Fiorentina-Napoli
2245 Inter Milan v Verona
2245 AS Roma v Torino
0 comments:
Post a Comment