Friday, 7 November 2014

STRAIKA MRISHO NGASSA ANGIA RASMI KWENYE REKODI YA FRIKA!


STRAIKA wa Klabu ya Yanga, Mrisho Ngassa, ameingia kwenye Rekodi rasmi za Afrika baada ya kuibuka kuwa Mfungaji Bora wa CAF CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2014 akiwa na Bao 6 akifungana na Wachezaji wengine Watatu.
NGASSAvRIO
Wengine waliofunga Bao 6 kwenye Mashindano hayo ambayo ES Setif ya Algeria iliibuka kuwa Mabingwa ni El Hedi Belameiri wa Setif, Firmin Ndombe Mubele wa AS Vita ya Congo DR na Haythem Jouini wa Esperance ya Tunisia.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia kwenye Chati aina hii kwenye Mashindano ya Barani Afrika.

CAF CHAMPIONZ LIGI 2014  
WAFUNGAJI BORA:
**Wote Bao 6
-Mrisho Ngasa [Yanga, Tanzania]
-Haythem Jouini [Espérance Tunis]                  
-Firmin Ndombe Mubele [AS Vita, Congo DR]                      
-El Hedi Belameiri [ES Setif, Algeria]                         
  
Ngassa alifunga Bao zake zote 6 dhidi ya Komorozine ya Visiwa vya Comoro waliyokutana nayo Raundi ya Awali ya CAF CHAMPIONZ LIGI mapema Mwaka huu.
Kwenye Mechi ya kwanza Jijini Dar es Salaam Ngassa alipiga Bao 3 Yanga waliposhinda 7-0 na marudiano huko Comoro, Ngassa tena alipiga Hetitriki Yanga ikishinda 5-1.
Raundi iliyofuata Yanga walikutana na waliokuwa Mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri na kubwagwa nje. 
Ngassa, mwenye Miaka 25, Mwaka 2009 aliwahi kwenda kufanya majaribio huko England na Klabu ya West Ham na vile vile huko Marekani na Klabu ya Seattle Sounders Mwaka 2011 na kucheza Mechi dhidi ya Manchester United waliyofungwa 7-0.
Hapa Nchini pia ameshazichezea Klabu za Kagera Sugar, Azam FC na Simba.

0 comments: