Zinedine Zidane sasa yuko huru kuifundisha Timu ya Vijana ya Real Madrid Castilla baada ya Kifungo chake cha Miezi Mitatu kutupwa hapo Jana.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, lilimfungia Zidane Mwezi uliopita kwa kutokuwa na Vyeti vinavyostahili kuwa Kocha huko Spain baada ya kupokea malalamiko toka kwa Chama cha Makocha cha Spain.
Ilidaiwa Zidane alikuwa na Leseni A ya UEFA ambayo huko Spain ni sawa na Daraja la Pili ambayo ni Daraja moja chini ya kiwango anachopaswa kuwa nacho Kocha anaefundisha Timu ya Daraja la Pili huko Spain, Segunda B.
Msimu uliopita Zidane alikuwa Msaidizi wa Kocha wa Timu ya Kwanza ya Real Madrid, Carlo Ancelotti, lakini mwanzoni mwa Msimu huu alipelekwa kuiongoza Real Madrid Castilla inayocheza Segunda B.
Hata hivyo, wakitarajia kuwepo malalamiko, Real haraka walimteua Msaidizi wa Zidane, Santiago Sanchez, kuwa Kocha Mkuu, ingawa ilikuwa wazi Kocha Mkuu ni Zidane.
Mara baada ya kufungiwa Zidane, Real ilikuja juu na kuapa kumpigani na kuamua kukata Rufaa kwa ACS, Administrative Court for Sport, Mahakama ya Michezo ya Spain, ambayo ilisimamisha Kifungo chake na kuitaka RFEF ipitie upya adhabu hiyo.
Uamuzi huu umemfanya Zidane awe huru kuiongoza Castilla kwa safari yao kwenda kucheza na Tudelano hapo Jumapili kwenye Mechi ya Segunda B.
0 comments:
Post a Comment