“Kwanza kabisa baada ya kukamatwa kwa basi la TFF, Malinzi aliagiza fedha zitoke huku na kulipa basi hilo. “Fedha alizotaka ni zile za Yanga za udhamini wa Azam TV kwa kuwa hawakuwa wamezichukua. Nikakataa kusaini, niliingia hofu kama Yanga wangezitaka fedha zao, tungezitoa wapi? “Kwake Malinzi ikawa ni nongwa, akaelezwa azungumze na mimi, akakataa kwa madai yeye ni rais hawezi kumbembeleza mtu, zoezi likakwama. “Mara ya pili, Malinzi tena akataka alituma wakaguzi wa mahesabu kupitia kampuni ya Whitehouse Coopers waje kukagua mahesabu ya bodi. “Kanuni na katiba ya TFF inasema anayetakiwa kukagua mahesabu ya bodi ni ile inayokagua mahesabu ya TFF.
Ile kampuni ambayo jamaa waliokuja walikuwa ni kabila la Wahaya, haikuwa inakagua mahesabu ya TFF. “Nikaona Malinzi alikuwa anavunja katiba, sikutaka aingie sehemu isiyo sahihi. Nikaona nimsaidie asije akaingia pabaya, nikagoma pia.” Dk Ndumbaro amesisitiza kuwa jambo la tatu ni taarifa za yeye kutaka kuwania urais wa TFF. “Rafiki zake wa karibu, hasa wapambe waliomzunguka ndiyo wamekuwa na hofu kubwa kwamba nikigombea basi yeye ataanguka kwa kuwa wanatambua hawako makini. “Sikuwahi kuwa na mpango huo, lakini kitu cha msingi hawapaswi kuhofia washindani. Ndiyo maana unaona wameamua kunifungia kienyeji. “Nakuhakikishia, hakuna watu makini wanaoweza kufanya kama ilivyofanya TFF kwa kushirikiana na kamati ya nidhamu.
“Watu wote wameona, serikali imeshangazwa, wadau wamepinga hilo na hiyo ni sehemu nyingine ambayo inaweza kuwa kipimo sahihi cha kuonyesha wao si watu makini hata kidogo.”
CHANZO Salehjembe.
0 comments:
Post a Comment