Sunday, 16 November 2014

KIMONDO YATOA SARE NA FRIENDS RANGERS NDANI YA KARUME

FRIENDS RANGERS
Kikosi cha Kimondo, leo kimeivuta shati Friends Rangers ambayo imekuwa ina kasi kubwa katika harakati ya kuwania kucheza Ligi Kuu Bara.

Katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, leo, Friends na Kimondo zilitoka sare ya bao 1-1.
Friends waliokuwa wenyeji walifanikiwa kupata bao katika dakika ya 11 kupitia Samwel Mathayo lakini wageni hao wakasawazisha katika dakika ya 23 kupitia Sunday William.

Friends inayofundishwa na Ally Yusuf  ‘Tigana’ ilipata nafasi ya kupata bao la pili baada ya kupata penalti lakini kiungo wake nyota, Almasi Mkinda akapiga na kupaisha.

Mechi inayofuatia, Friends itaivaa African Sports mjini Tanga

0 comments: