KLABU ya Arsenal inakabiliwa na baa la majeruhi, baada ya Jack Wilshere naye kutakiwa kuwa nje kwa miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu jana.
Na kocha Arsene Wenger atalazimika kuingia sokoni Januari kununua wachezaji ili kupoza maumivu ya tatizo la majeruhi kikosini mwake.
Wilshere amefanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto baada ya kipigo cha Manchester United cha mabao 2-1 Uwanja wa Emirates Jumamosi iliyopita. Na Nahodha, Mikel Arteta pia anaweza asicheze tena mwaka huu baada ya kuumia Arsenal ikishinda 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund.
Wilshere ameposti picha hii baada ya kufanyiwa upasuaji
Kuuminia kwa Wilshere kunamfanya kocha Arsene Wenger awakose viungo wote watatu tegemeo, Aaron Ramsey, Mathieu Flamini na Tomas Rosicky.
Baada ya upasuaji huo, Wilshere akaposti picha Instagram akiwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba zoezi limekwenda vizuri.
"Kifundo cha mwishowe kilihitaji upasuaji," ameandika. "Zoezi limekwenda vizuri na asante kwa mkuu James Calder (mpasuaji)!
Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia na anatarajiwa kurejea kikosini Arsenal kabla ya Machi, mwakani
0 comments:
Post a Comment