MATOKEO:
Jumapili Novemba 23
Crystal Palace 3 Liverpool 1
Hull City 1 Tottenham 2
Tottenham walitoka nyuma kwa Bao 1 walipocheza ugenini na kuifunga Hull City iliyocheza Mtu 10 Bao 2-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
Hull walitangulia kufunga katika Dakika ya 9 kwa Bao la la Shuti la mbali la Jake Livermore.
Lakini Hull City walikatwa maini katika Dakika ya 50 baada ya Kiungo wao Gaston Ramirez kutolewa kwa Kadi Nyekundu kwa kurudishia alipochezewa Rafu na Jan Vertonghen na huo ukawa mwanya kwa Tottenham kurudi kwenye Mechi.
Harry Kane akaisawazishia Tottenham Dakika ya 61 baada ya Frikiki ya Christian Eriksen kugonga mwamba na kumrudia na alikuwa Christian Eriksen aliewapa ushindi kwa Shuti la Mita 20 katika Dakika ya 90.
Matokeo haya yamewapandisha Tottenham hadi Nafasi ya 10 na kuwaacha Hull wakiwa na ushindi wa Mechi 1 tu katika Mechi 11 zilizopita.
VIKOSI:
Hull City: McGregor; Elmohamady, Dawson, Davies, Robertson; Huddlestone, Livermore; Ben Arfa, Ramírez, Brady; Jelavic
Akiba: Rosenior, Chester, Meyler, Hernandez, Sagbo, Harper, Quinn
Tottenham: Lloris; Dier, Fazio, Vertonghen, Davies; Eriksen, Mason, Dembele, Lamela; Soldado, Kane
Akiba: Chiriches, Lennon, Paulinho, Vorm, Stambouli, Ceballos, Ball
LIVERPOOL HOI, YAPIGWA 3 NA PALACE, NI KIPIGO CHA 3 MFULULIZO!
- D
LIVERPOOL, wakicheza Ugenini huko Selhurst Park Jijini London, waliongoza baada ya Sekunde 90 tu kwa Bao la Rickie Lambert lakini wakajikutwa wakibwagwa chali na kukung’utwa Bao 3-1 na Crystal Palace katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Palace walisawazisha Bao katika Dakika ya 17 kwa Bao la Dwight Gayle alienasa Shuti la Yannick Bolasie lililopiga Posti na kumrudia.
Kipindi cha Pili Dakika ya 78 Joe Ledley aliwapeleka Palace mbele 2-1 na kisha Dakika 3 baadae Frikiki ya Mita 25 ya Mile Jedinak ilitinga na kuwapa Palace Bao lao la 3.
Mechi hii imewaacha Wadau wa Liverpool wakihoji uchezaji wa Nahodha wao Steven Gerrard na Raheem Sterling ambao wameonyesha kufifia mno.
Kipigo hiki cha Leo kinawafanya Liverpool wawe wamechapwa Mechi 3 mfulilizo za Ligi na kushinda Mechi 1 tu kati ya 5 zilizopita na kuwaacha wakiwa Nafasi ya 12 wakiwa Pointi 18 nyuma ya Vinara Chelsea.
Katika Mechi zao 2 zilizopita, Liverpool wametandikwa 2-1 na Chelsea na 1-0 na Newcastle.
VIKOSI:
Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann, Delaney, Ward, Bolasie, Jedinak, Ledley, Puncheon, Chamakh, Gayle
Akiba: Hangeland, Campbell, Zaha, Hennessey, Johnson, McArthur, Bannan.
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Lovren, Skrtel, Johnson, Allen, Gerrard, Coutinho, Sterling, Lambert, Lallana
Liverpool: Mignolet, Manquillo, Lovren, Skrtel, Johnson, Allen, Gerrard, Coutinho, Sterling, Lambert, Lallana
Akiba: Brad Jones, Toure, Moreno, Lucas, Can, Borini, Markovic.
REFA: Craig Pawson
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Novemba 24
2300 Aston Villa v Southampton
Jumamosi Novemba 29
1545 West Brom v Arsenal
1800 Burnley v Aston Villa
1800 Liverpool v Stoke
1800 Man Utd v Hull
1800 QPR v Leicester
1800 Swansea v Crystal Palace
1800 West Ham v Newcastle
2030 Sunderland v Chelsea
Jumapili Novemba 30
1630 Southampton v Man City
1900 Tottenham v Everton
Jumanne Desemba 2
2245 Burnley v Newcastle
2245 Leicester v Liverpool
2245 Man Utd v Stoke
2245 Swansea v QPR
2300 Crystal Palace v Aston Villa
2300 West Brom v West Ham
Jumatano Desemba 3
2245 Arsenal v Southampton
2245 Chelsea v Tottenham
2245 Everton v Hull
2245 Sunderland v Man City
MSIMAMO:
0 comments:
Post a Comment