Sunday, 16 November 2014

UONGOZI WA MBEYA CITY WAKANUSHA TAARIFA ZA KUBWAGA MANYANGA KWA MWAMBUSI

 Juma mwambusi akiwana Katibu mkuu wa mbeya city emmanuel kimbe  na viongozi wengine wa timu hiyo

Uongozi wa Mbeya City umesema haujui lolote kuhusiana na taarifa zinazozagaa kwa kasi kwamba Kocha Juma Mwambusi amebwaga manyanga.

Taarifa hizo zilizagaa kwa kasi kwenye mitandao kwamba kutokana na mwenendo mbaya, Mwambusi ameamua kujiuzulu.
Lakini Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe amesema Mwambusi bado anaitumikia timu hiyo.
“Kweli sisi hatuna hizo taarifa, Mwambusi bado ni kocha wetu.
“Nimekuwa na mawasiliano naye saa chache zilizopita na hakuna taarifa za kujiuzulu,” alisema Kimbe.
Katika mechi saba za mzunguko wa kwanza, Mbeya City tayari imepoteza mechi nne.

Wakati katika mechi 26 za msimu uliopita, City ilipoteza tatu tu.

0 comments: