MUUNGANO wa Vyama vitano vya siasa umewataka wanasiasa kuacha kumpiga Mwenyekiti wa Kampuni ya IPTL na PAP, Harbinder Saign Sethi, kwamba amehusika na upotevu wa sh bilioni 200 katika Akaunti ya Escrow. Vyama hivyo vitano ni Chana Cha Kijamii (CCK), Chama cha wa Kulima (AFP), Chama cha Sauti ya Umama (SAU), UMD na Demokrasia Makini. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu chama cha SAU, Ali Kaniki, alisema wanapenda kuwaonya wanasiasa hao kuhusu madhara yanayoweza kusababishwa na kauli zao na mienendo yao isiyofaa ya kuingilia na kujaribu kutabiri matokeo ya ripoti ya Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Seikali (CAG). Alisema hivyo kwa sababu kupiga vita muwekezaji huyo watakuwa wanamuonea, wakati wahusika wakuu waliohusika na ufisadi huo wanatambulika, ambao ni viongozi wa serikali. Kaniki, alisema kiongozi wakwanza kabisa nayepaswa kuwajibika ni Waziri Mkuu Piter Mizengo Pinda ambaye tangu kugundulika kwa sakata hilo ameshindwa kuchukua hatua za haraka kulipatia ufumbuzi.
“Umoja wetu wa vyama vitano vya siasa vilivyosajiliwa, hatuna tatizo na matokeo au mambo yalivyogumdulika kwenye ukaguzi huo, tatizo lipo kwenye kuanza kuwaaminisha wananchi kuwa suala hilo lina madudu ndani yake ili hali bado matokeo hayajatangazwa hadharani,”alisema Kaniki.
Alisema kumekuwa na upotoshaji umma kutokana na baadhi ya wanasiasa wengine wakidai kuwa fedha zilizoko katika Akaunti ya Escrow kuwa ni zilikuwa za umma huku upande mwingine ukisema hazikuwa za umma bali za IPTL . Alisema kuhifadhiwa kwa fedha hizo katika Akaunti ya Escrow kulitokana na mgogoro baina ya wabia wa IPTL, ambao walikuwa ni kampuni ya Mechmar Corporation (Malaysia), Berhad na VIP Engineering & Marketing Limited (VIP). Kaniki, alisema hayo yote ni mambo ambayo yanawachanganya wananchi ambao kwa namna moja au nyingine, wasiwe na uelewa mpana wa kubaini nani anasema ukweli katika sakata hilo.
Alisema kwa hiyo wanaomba wanasiasa na wananchi kwa ujumla kuwa wavumilivu na kusubiri ripoti hiyo isomwe hadharani pale Bungeni ili waone ni hatua gani zitachukuliwa kwa watakaothibitika kuwa na makosa. Naye Katibu Mkuu wa CCK, Lenatus Muhabhi, alisema kutokana na tabia za wanasiasa wa aina hii wenyekupenda kundandia mada wanaweza kuwafurahisha baadhi ya wawekezaji kudhani kuwa Tanzania haina mazingira rafiki ya uwekezaji kwa sababu ya siasa mbovu. Aidha, kuna taarifa kuwa mwekezaji huyo wa IPTL ameombwa na anchi za jirani ambazo ni Burundi, Rwanda na Kenya lwemda kuwekeza katika kuzalisha umeme wa megawati 200.
Muhabhi, alisema hiyo inaashiria kwamba mwekezaji huyo amaweza akaamua kuhama kutoka Tanzania na kwenda kuwekeza katika nchi ambayo inaona umuhimu wake. Alisema Watanzania wamekuwa ni kama wanampiga vita baadala ya kuangalia fursa alizozileta na jithada alizozifamya ili kuokoa sekta ya umeme hapa nchini.
Na Mwandishi wetu
0 comments:
Post a Comment