Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, ameutaka uongozi wa
Wekundu hao wa Msimbazi kusajili wachezaji 25 tu msimu ujao wa ligi kuu ambapo
amependekeza kuwa na makipa watatu.
Loga amekabidhi ripoti yake hivi karibuni kabla ya kwenda nchini
kwao Croatia kwenye mapumziko huku akisubiri majibu iwapo ataitwa kuendelea na
timu hiyo au la ambapo mkataba wake unaisha Juni, mwaka huu.
Akizungumza na Championi Jumatano, Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel
Kamwaga, alisema ripoti hiyo ya kocha aliyoiwakilisha imependekeza kusajili
wachezaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukabidhi majina ya wachezaji
wanaotakiwa na wasiotakiwa kubaki msimu ujao ambapo idadi kamili anayoitaka ni
wachezaji 25.
“Loga amependekeza wachezaji kadhaa wabaki ambao anaona wanafaa
kuwatumia kwa ajili ya msimu ujao ambapo amesema anataka wachezaji 25 tu katika
timu nzima na iwapo idadi itaongezeka basi itakuwa ni ya viongozi.
“Anahitaji kila nafasi iwe na wachezaji wawili huku kwa upande wa
makipa amependekeza waongezwe wawili ili kuwa na jumla ya makipa watatu pamoja
na Ivo Mapunda.
“Kuna nafasi mbalimbali ambazo ametaka zisajiliwe, hivyo
tutaangalia mahitaji yake iwapo nafasi hizo kuna wachezaji wa Tanzania
watakaofaa au kuangalia nje ya nchi kwa kuwa kuna namba nyingine ni lazima
tuzipate nje.
“Pia kuna baadhi ya wachezaji ambao amewapendekeza wasajiliwe kutoka katika timu mbalimbali za ligi kuu, lakini siwezi kuwataja kwa kuwa ni mapema mno,” alisema Kamwaga.
0 comments:
Post a Comment