Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma imetawazwa rasmi kuwa bingwa wa mpira wa Pete wa Mashindano ya Mei Mosi 2014.
Utumishi imefanikiwa kuwa bingwa
baada ya kuisambaratisha timu ya Wizara ya Uchukuzi kwa ushindi wa
magoli 33 dhidi ya 21. Mchezo huo wa fainali ulifanyika katika uwanja wa
Jamhuri mjini Morogoro.
Katika mchezo huo mchezaji Fatuma
Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais Utumishi ndiye aliyekua tishio kwa
kuongoza wachezaji wa timu yake kufanikisha ushindi huo.
Mchezaji Subira Jumanne (WA) wa
Uchukuzi akizungumzia hali ya mchezo baada ya mpira kumalizika alisema
kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wao walikua wamejiandaa vyema.
“Naamini wakati wa mashindano
mengine tutafanya vizuri kwa kujiandaa vyakutosha, asiyekubali kushindwa
si mshindani” Subira alisema.
Wakati huohuo, Fatuma Machenga
(GS) wa Utumishi ameibuka kuwa mfungaji bora wa mpira wa Pete katika
mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa kufunga jumla ya magoli 136.
“Tutahakikisha kuwa mwakani tunapambana zaidi kwa kufanya mazoezi ya kutosha ili kutetea ubingwa wetu” Machenga alisema.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma imenyakua kombe hilo lililokuwa likishikiliwa na timu
ya Wizara ya Ulinzi iliyokuwa bingwa katika mashindano yaliyopita Mwaka
2013.
Mshindi wa Pili kwa mwaka 2014 ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mashindano hayo yalimalizika jana katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Na James Katubuka
0 comments:
Post a Comment