Muadhirika
wa tukio la moto Dick Lulandala akiwa na rafiki yake Luka wakiangalia
ofisi yake inayojihusisha na uchapishaji wa mabango , fulana baada ya
kuteketezwa na moto ambapo hakuna hata kimoja kilichonusurika
Jeshi la
polisi lilifanya kazi nzuri kwa kudhibiti mali zilizonusurika, hata
hivyo kijana mmoja aliwekwa chini ya ulinzi kwa kujaribu kuiba
Kikosi cha zimamoto kikifanya kazi kwa bidii kudhibiti moto huo ingawa waliishiwa na maji..
Hapa
iringa moto unaosadikiwa kuwaka kutokana na itilafu ya umeme umeteketeza
mali katika jengo moja lililopo mtaa wa benbela gangilonga katika
manispaa ya iringa .jengo hilo linalomilikiwa na Shirika la nyumba
limezungukwa na ofisi pamoja na maduka ya bishara, Moto umesababisha
madhara makubwa na ulizimwa na kikosi cha zimamoto kwa kushirikiana na
wananchi , Ally Britoni ni mwenyekiti wa mtaa huo na ameieleza kwanza
jamii na mjengwa blog kuwa moto ulianza kwa kuziona cheche majira ya saa
nne kasoro za usiku lakini pia amewashukuru
kikosi cha zimamoto iringa kwa kuitikia wito kwa haraka.Dick Lulandala
ni swahiba yangu aliyekuwa katika hali ya huzuni kwa kuteketea kwa
mashine za uchapishaji zenye gharama kubwa sana. Mjengwa blog na kwanza
Jamii inawapa pole wote walioathiliwa na moto huo....
H ABARI na Edward Majura
Sagini
0 comments:
Post a Comment