Mkurugenzi wa
Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akitoa ufafanuzi kwa
Wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa
Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma
ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo.
Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza
kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha
katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi
mkuu.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu
hoja mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.
Akijibu
moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika
upatikanaji wa Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji
wa Katiba umemelizika na kuonekana kuwa na mapungufu machache
yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha katiba hiyo.
“Mchakato
wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini
kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara
iweze kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.
Akifafanua
zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa
kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana
tofauti na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya
marekebisho hayo mapema na kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya
kuidhinishwa.
Aidha
Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club ya
Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya
Club yao kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini.
Na Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini (WHVUM)
0 comments:
Post a Comment