Inashangaza:
Petr Cech akitembea na Nathan Ake (katikati) na Marco van Ginkel kuelekea
katika mazoezi.
JOSE
Mourinho ameanza maandaliza ya mechi ya kesho ya nusu fainali ya pili ya UEFA dhidi
ya Atletico Madrid, huku ikishangaza kumuona mlinda mlango namba moja wa
Chelsea, Petr Cech akifanya mazoezi.
Cech
aliteguka beka katika mchezo wa kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila
kufungana Vicente Calderon na Mourinho alithibitisha wiki iliyopita kuwa kipa
huyo anahitaji upasuaji ili kurudisha bega katika hali yake.
Nyota
wa samba: Willian, David Luiz, Ramires na Oscar wakielekea katika uwanja wa Coham tayari
kwa mazoezi.
Haikuwa
rahisi kumouna Cech leo hii ambaye alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi
mitatu, hivyo imeshangaza kumuona mchezaji huyo akiwa miongozi kwa wachezaji
waliofanya mazoezi leo hii.
Alipoulizwa
kama yuko imara kwa mechi ya kesho, alitabasamu na kusema “Ndiyo”, lakini
alienda zake na kujiunga na wenzake.
Cech alionekana akifanya mazoezi mepesi leo hii,
na makipa wenzake Mark Schwarzer, Henrique Hilario na Mitchell Beeney walipoanza mazoezi na kocha wa makipa, Christophe
Lollichon, Cech alikaa pembeni.
Mbali na Cech, wachezaji wengine waliokuwa
majeruhi, Samuel Eto`o, nahodha, John Terry, na Eden Hazard nao wamefanya
mazoezi leo hii kujiandaa na kipute cha kesho.
0 comments:
Post a Comment