Muda wa mwisho uliowekwa na Marekani wa mpango wa mashariki ya kati umemalizika.
Mchakato huo unaonekana kugonga mwamba .Mazungumzo yao yalivunjika pale Israeli ilipoukataa mpango wa amani baina ya makundi makuu mawili ya Wapalestina wa kuunda serikali ya Umoja na hasira ya wapalestina kutokana na ujenzi wa Israeli wa makazi mapya katika
maeneo ynayokaliwa .
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amekasirishwa na kitendo cha Israeli kuendelea kujenga maakazi ya Wayahudi na Palestina kupendelea kuunda serikali ya umoja na kundi la Hamas.
Hatahivyo haja kubali kushindwa anatumia maneno kama ''kusitishwa kwa muda kwa harakati za kutafuta amani''.
Kuna uwezekano kuwa huenda Marekani itafuatilia kwa karibu yanayoendelea huku ikishinikiza kurejelewa kwa mchakato wa kutafuta Amani.
Hatahivyo baadhi ya washirika wa Marekani katika mazungumzo hayo wanamasema kuwa muda wa kuleta Amani umekwisha.
Viongozi wa nchi za Ulaya na matiafa ya Kiarabu wameunga mkono juhudi za John Kerry katika kujaribu kulitafutia suluhu tatizo la Israil na Palestina na kushikilia msimamo kwamba Marekani ndio taifa pekee lenye uwezo mkubwa wa kufanikisha mchakato huo.
0 comments:
Post a Comment