KAMA
anavyotamba katika ngumi za kulipwa hadi sasa akiwa hajapoteza pambano
licha ya kupigana na mabondia wakali duniani, Floyd Mayweather anataka
kununua klabu ya mpira wa kikapu Marekani, inayomilikiwa na milionea
anayekabiliwa na kashfa ya ubaguzi.
Hakuna
ajabu kwa mkali huyo wa kutupa mikono kwenye miili ya wenzake,
anayekwenda kwa jina la utani Money Mayweather juu ya hilo, kwa sababu
ana uwezo kifedha.
Floyd
Jnr anataka kutoa dola za Kimarekani Milioni 40 ambazo ni sehemu tu ya
pato lake la pambano la Jumamosi wiki hii, atakalolipwa dola bilioni 1.8
ili kuinunua Los Angeles Clippers.
Kuhusu
Clippers, ambayo mmiliki wake Donald Sterling amefungiwa maisha
kujihusisha na masuala ya mpira wa kikapu baada ya kupatikana na hatia
ya kuwatolea maneno ya kibaguzi watu weusi wa timu yake wakiwemo
wachezaji, Mayweather amesema: "Ninataka kuinunua Clippers? Ndiyo.
Naweza kuwaunganisha pamoja watu ambao watakuwa tayari.
"Kununua
timu ya Ligi Kuu ya kikapu ni kitu fulani ambacho nataka kuongeza
katika kampuni yetu inayokua kwa kasi ya Mayweather Promotions, ambayo
sasa si kwa ajili ya ngumi tu, bali tunajihusisha pia na mavazi, muziki
na sinema,"alisema.
Kifungo
cha maisha: Mmiliki wa Los Angeles Clippers, Donald Sterling hawezi
kujihusisha na masuala ya mpira wa kikapu baada ya kutoa kauli ya
kibaguzi hadharani
0 comments:
Post a Comment