Friday, 25 April 2014

MSD YASHIRIKI MAONESHO YA KITAIFA YA SIKU YA MALARIA DUNIANI

KATIKA HOTELI YA HYATT JIJINI DAR ES SALAAM LEO




 Nembo ya Bohari ya Dawa (MSD)

 
Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam, Florida Sianga (wa pili kulia), akiwaelekeza jambo waandishi wa habari waliotembelea banda la MSD katika maonesho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Kitaifa Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.Waliokaa kutoka kushoto ni Balozi wa malaria wa MSD, Lameck Kipiliango na Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.


 Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam, Florida Sianga (wa pili kulia), akiwaelekeza jambo waandishi wa habari waliotembelea banda la MSD katika maonesho ya Siku ya Malaria Duniani yaliyofanyika Kitaifa Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.Waliokaa kutoka kushoto ni Balozi wa malaria wa MSD, Lameck Kipiliango na Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.



 Balozi wa Malaria wa MSD, Lameck Kipiliango (kushoto), akizungumza na wanahabari (hawapo pichani), waliotembelea banda la MSD. Kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid.


Maofisa wa MSD wakipanga bidhaa zao katika banda lao kwenye maonesho hayo. Kutoka kushoto ni Ofisa Habari wa MSD, Etty Kusiluka, Balozi wa Malaria wa MSD, Lameck Kipiliango, Ofisa Mwandamizi wa Huduma kwa Wateja wa MSD, Idd Abeid na Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam, Florida Sianga

Na Dotto Mwaibale



PAMOJA na kuwepo kwa malalamiko ya kukosekana kwa dawa za malaria katika Hospitali mbalimbali hapa nchini Bohari ya Dawa (MSD), imesema ina dawa za kutosha.


Hayo yalibainishwa na Balozi wa Malaria wa MSD,  Lameck Kipiliango  wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la MSD katika maonesho ya  maadhimisho ya siku ya malaria duniani, ambayo kitaifa yamefanyika katika Hoteli ya Hyatt Dar es Salaam leo.


Akifafanua zaidi,  Kipiliango alisema wamekuwa wakishindwa kuweka makisio ya kiasi cha dawa wanachohitaji na hivyo kujikuta zikiwaishia kabla ya muda na hivyo kuonekana kama kuna upungufu kwa nchi nzima jambo ambalo sio la kweli.


Kuhusu MSD kuchaguliwa kama balozi wa malaria tangu mwaka jana, alisema wamekuwa wakitelekeza shughuli mbalimbali ikiwemo mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi wao kuhusu ugonjwa huo.


Kama vile haitoshi alisema wamekuwa wakimpatia kila mfanyakazi chandarua kulingana na idadi ya familia yake kwa nia ya kuielimisha jamii inayowazunguka umuhimu wa kutumia chandarua katika kujikinga na malaria.


Aidha kupitia wafanyakazi wao wamekuwa wakitoa elimu kupitia kanda tano walizozigawa katika maeneo mbalimbali nchini.


Naye Ofisa Huduma kwa Wateja wa Bohari ya Dawa (MSD), Kanda ya Dar es Salaam, Florida Siyanga , alizitaja baadhi ya changamoto ambazo  wamekuwa wakikabiliana nazo katika usambazaji wa dawa ni uhaba wa magari na ubovu wa miundombinu ambapo katika maeneo mengine wanalazimika kutumia kutumia pikipiki au mitumbwi.


Katika kutatua kasoro hizo, wito wake Siyanga alitaka watumishi kupata mafunzo ya namna ya kuagiza dawa ili ziweze kuwatosha katika msimu mzima wa mwaka ili wananchi wazipate kwa wakati.

0 comments: