Balozi wa
Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Mhe. Modest
Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya watu wa China-Geneva, Liu
Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa ILO hii leo na
kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo balozi huyo China UN
mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika Kusini, Balozi wa Togo,
Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa Rwanda, wawakilishi wa
Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Watanzania waishio
Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose Mero.
Mke wa
Balozi Mero, Rose Mero akisalimiana na ujumbe wa Ubalozi wa Denmark.
pamoja nao ni Balozi Modest Mero na Balozi wa Dernmark-UN.
Balozi Mero akijumuika na mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria katika tafrija hiyo.
Familia ya Balozi Mero katika picha ya Pamoja.
Wanawake mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mke wa Balozi Mero.
Balozi Mero alitoa hotuba ambayo ilielezea historia, maendeleo, na maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya, Hotuba hiyo pia iliweza kubaiinisha wazi ni vipi Tanzania na Watanzania wameweza kumudu kurumu katika muungano huo kwa miaka 50 sasa.
Afisa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania UN, Hamisa Mkoma akiwa na Mke wa Balozi wa Tanzania UN, Mama Rose Mero
Balozi Modest Mero akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa katika Ubalozi wa Tanzania UN mjini Geneva.
Wageni mbalimbali waliohudhuria tafrija hiyo.
(J M)
0 comments:
Post a Comment