Baraka Mpenja , Dar es salaam
MABADILIKO
ya mfululizo katika benchi la ufundi imetajwa kuwa moja ya sababu ya
Wekundu wa Msimbazi kufanya vibaya msimu wa 2013/2014 uliomalizika
aprili 19 mwaka huu kwa timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 na watani zao
wa Jadi, Yanga SC.
Simba walimaliza ligi wakiwa katika nafasi ya 4 baada ya kujikusanyia pointi 38 pekee katika michezo 26.
Ally Mayay Tembele, beki na nahodha
wa zamani wa Yanga sc na sasa kocha wa mpira wa miguu amesema kuwa
kubadili benchi la ufundi mara kwa mara kunaleta athari ya moja kwa moja
katika kikosi.
“Kila mwalimu ana falsafa yake,
kwahiyo unapobadili kocha ujue kabisa unaleta mfumo mpya katika klabu
ambao utahitaji muda ili wachezaji wazoee”.
“Msimu wa 2011/2012 alikuwepo kocha
Mserbia Milovan Circovic, baadaye akaja mfaransa Patric Liewig. Akiwa
ameshaanza kuijenga Simba ya vijana na sasa wanaanza kumuelewa,
akaondolewa na kuletwa Abdallah Kibadeni. Hawa ni walimu watatu tofauti
na wana aina yao ya ufundishaji”
“Wachezaji ndani ya muda mfupi
walijikuta wakilishwa mifumo tofauti. Sasa walishindwa kushika kwa
haraka kwasababu wakianza kuzoea kunatokea mabadiliko”,
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment