Tanzania iko katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mfumo wa National Electronic Single Window System, makati bio ya mfumo huu yataanza mwezi June 2014, utarahisisha ufanyaji biashara na kuchangia kainua uchumi wa Tanzania … Mradi huu ni sehemu ya Mpango wa Matokeo Makubwa sasa ( Big Result Now) unasimamiwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa niaba ya wadau wote na utanufaisha watumiaji wa bandari zetu zote, viwanja vya ndege, mipaka yote ya Tanzania. Mfumo huu unatarajiwa kupunguza muda wa mizigo kukaa bandarini na hivyo bidhaa kuingia katika mzunguko wa uchumi haraka.
Wadau
wa Port Community System wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kikao leo, Tanzania iko katika hatua ya utekelezaji wa mfumo wa National
Electronic Single Window System, mfumo huu utaanza kutumika June 2014
na kurahisisha ufanyaji biashara na kuchangia kainua uchumi wa Tanzania.
Mkurugenzi
wa ICT – TPA Ndg. Phares Magesa akibadilishana mawazo na mwakilishi
toka ofisi ya Waziri Mkuu ambao wanafuatilia maendeleo ya mradi huo.
Wadau wa Port Community wakiwa katika mkutano wao ili kuupitia na hatimaye kuupitisha rasmi mfumo huo.
Mwenyekiti
wa wadau Ndg. Igogo kulia akijadiliana jambo na Ndg. Magesa ambaye ni
Meneja wa mradi huo kwa niaba ya wadau wote wa Bandari, kushoto ni
Meneja Mkuu wa kampuni ya Phaeros Group ya Ubelgiji ambao ndio
watengenezaji wa mfumo huo.
0 comments:
Post a Comment