Ikiwa
imebakia siku moja kabla ya kuadhimisha siku ya Malaria Duniani, wakazi wa
Iringa wametakiwa kuwa makini na ugonjwa huu hatari unaoua mamia ya watu kila
mwaka.
Akizungumza
na mtandao wa wandishi wa habari
ofisini kwake Mratibu wa kuthibiti malaria Manispaa ya Iringa Dokta Nicolous
Ntabaye alisema kuwa maadhimisho hayo ya kuthibiti malaria dunia huwa
yanafanyika kila tarehe 25 Aprili na kusema thumuni la kufanya maadhimisho hayo
ni pamoja na kuthibiti uongezekaji wa ugonjwa huo hatari wa malaria.
“sisi
kama Manispaa tumejipanga vizuri kwa kuwaasa wananchi wetu kuwa waangalifu na
ugonjwa huu wa malaria na mikakati tukiyojiwekea kwa wananchi wa Iringa ni
pamoja na kuwaasa wahakikishe mazingira yanayowazunguka yawe safi na salama,
mama wajawazito wahakikishe wanatumia vidonge vya SP ili kumkinga mtoto aliyeko
tumboni asipatwe na malaria pia kuendelea kutumia vyandarua vilivyowekwa dawa
na endapo mtu akijua ana dalili za maralia ahakikishe anawahi kwenda hospitali
akapatiwe matibabu mapema,” alisema Dokta.
Hata
hivyo ametoa wito kwa wamama wajawazito kuhakikisha wanapewa vidonge vya SP
dozi mara tatu kwa miezi yake tisa mpaka atakapojifungua ili kumfanya mtoto
azaliwe katika afya njema na asipatwe na ugonjwa wa malaria kwa kufanya hivyo
uongezekaji wa malaria utapungua Nchini.
Maadhimisho
hayo ya ugonjwa wa Malaria yanatarajia kufanyika kesho huku kauli mbiu ikiwa “wekeza
katika muda wa baadaye, tokomeza Malaria”.
HABARI NA
DIANA BISANGAO , IRINGA
0 comments:
Post a Comment