Balozi
wa Tanzania chini Nigeria Mh. Daniel Ole Njoolay akifungua kongamano
la Biashara na uwekezaji katika Hoteli ya Serena jijini Abuja Nigeria
ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar zilizoandaliwa na ofisi ya ubalozi wa Tanzania
nchini Nigeria.
Mjumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi wa TTB Bibi Teddy Mapunda akizungumza wakati
Alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu vivutio vya utalii Tanzania katika
kongamano la biashara na uwekeza jijijini Abuja nchini Nigeria.
Mh.
Daniel Ole Njoolay, Balozi wa Tanzania nchini Nigeria akikata keki huku
akishuhudiwa na mwakilishi wa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan (wa
pili kulia) na baadhi mabalozi wanaowakilisha nchi zao Nigeria katika
tafrija iliyotayarishwa na ubalozi wa Tanzania.
Kikundi
cha ngoma za asili cha Abuja Nigeria kikitoa burudani ya ngoma katika
tafrija kusheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar .
……………………………………………….
Na Geofrey Tengeneza – Abuja Nigeria
Jumuiya
ya wafanyabiashara, wawekezaji na wananchi wa Nigeria kwa ujumla,
wameombwa kuja kuwekeza na kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
vinavyopatikana nchini Tanzania
Hayo
yamesemwa na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mheshimiwa Daniel Ole
Njoolay katika maadhimisho ya miaka hamsini 50 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar (Tanzania) yalioandaliwa na ofisi ya ubalozi waTanzania
nchini Nigeria na kufanyika katika Hoteli ya Sheraton jijini Abuja.
Akiongea
wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo la Biashara na Uwekezaji, Njoolay
alisema Tanzania inajivunia muungano wake ulioasisiwa na Hayati Baba
waTaifa Mwl Julius Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume muasisi wa
Zanzibar mnamo tarehe 26 April, 1964 ambao sasa umetimiza miaka 50.
“Watanzania
tunajivunia sana muungano wetu kwani ni wakipekee sana hapa barani
Afrika, na ni muungano uliodumu kwa muda mrefu zaidi kuliko muungano
wowote ule Barani Afrika”…alisema BaloziNjoolay.
Akizungumzia
kuhusu fursa za biashara Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa
TANTRADE Bwana Edwin Rutageruka alisema kwamba mahusiano ya kibiashara
kati ya nchi hizi mbili yameendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kwamba
Tanzania imedhamiria kuendelea kukuza biashara kati yake na Nigeria.
Akiwasilisha
mada kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania vilivyomo katika orodha ya
maajabu 7 ya asili barani Africa, Mkurugenzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya
TTB Bibi Teddy Mapunda alisema pamoja na vivutio vitatu (3) vya utalii
ambavyo ni Mlima Kilimanjaro, Crater ya Ngorongoro na Hifadhi yaTaifa ya
Serengeti, Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi zaidi na vya
kipekee na akabainisha kuwa imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika
kutangaza vivutio vyake saba vya asili ambavyo pamoja na vile vilivyomo
katika maajabu Saba ya asili barani Afrika, vivutio vingine ni hifadhi
ya taifa ya Ruaha, Hifadhi yaTaifa ya Kituro, hifadhi yaTaifa ya Gombe
na Pori la akiba la Selous.
Amewakaribisha wananchi wa Nigeria kutembelea Tanzania na kujionea uzuri na upekee wa vivutio vya Tanzania.
Kongamano
hilo lililohudhuriwa na takribani wawekezaji na wafanyabiashara kutoka
Nigeria mia moja lilifuatiwa na tafrija iliyofanyika usiku katika hoteli
hiyo na kuhuidhuriwa na waalikwa takribani 350 wakiwemo Mabalozi wa
mataifa mbalimbali nchini Nigeria, wageni kadhaa mashuhuri na baadhi ya
watanzania waishio nchini Nigeria.
ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA
Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria.
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria.
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Na Andrew Chale
MBUNIFU
mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki
aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho kubwa la mavazi ya
ubunifu lililokuwa maalum kwa ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.
Onyesho
hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota
tano ya Sheraton Abuja, usiku wa April 25, huku likiudhuriwa na watu
wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na
balozi anayewaiwakilisha Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.
Akizungumza
na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria, Asia Idarous
ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa
kuandaa onyesho hilo maalum, kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye
nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.
“Hii
ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika
na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya
ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja
nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema
baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai
kutoka Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria
na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.
Sherehe
hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi
mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho
hilo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda,
Fatma Mwinyi, Salma Maulid na wengine wengi.
“Utanzania
wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha ndani na nje
ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza
tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao
‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.
Nigeria
ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa
mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na
mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija na hata Taifa
hilo kuwa juu kiuchumi.
0 comments:
Post a Comment