Kamishna
wa elimu katika jimbo la Borno nchini Nigeria amesema kuwa wasichana 14
zaidi wamefanikiwa kutoroka katika mikono ya wanamgambo wa kiislamu
waliowatekanyara Jumatatu usiku.
Musa Inuwo Kubo, amesema wasichana 44 sasa wamewatoroka watekaji hao na kwamba wasichana wengine 85 hawajulikani walipoVikosi vya Usalama,makundi ya vijana wa kuweka usalama mitaani pamoja na familia za wasichana hao wanaendelea kuwatafuta.
Wasichana hao wanaaminika kutekwanyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa wasichana wamekuwa wakitekwanyara na kundi hilo lakini sio katika kiwango kama cha sasa.
Amesema kuwa wapiganaji hao wanapinga kuwepo kwa elimu ya kidunia na kwamba wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu.CHANZO BBC
0 comments:
Post a Comment